Burudani

Wanawake walionyanyaswa kingono na R. Kelly wafunguka mazito ‘alituvua nguo na kuanza kutu..’ (+video)

Ikiwa bado skendo ya mfalme wa muziki wa RnB duniani, R. Kelly ya kuwanyanyasa kingono wasichana miaka ya 2000’s, bado haijachukuliwa hatua yoyote kisheria, hatimaye kituo cha runinga cha LifeTime kimekuja na documentary maalumu iitwaayo ‘Surviving R. Kelly‘ ambayo inawaonesha wanawake wote waliowahi kunyanyaswa kingono na gwiji huyo wa R’n’B miaka ya nyuma.

Image result for R Kelly and sexual abuse
R. Kelly

Kwenye Documentary hiyo, ambayo imeanza kuruka jana kupitia kituo hicho. Wanaonekana wanawake sita akiwemo aliyekuwa mke wake, Andrea Kelly ambaye ameeleza kuwa alishawahi kutishiwa kuuawa na R. Kelly.

Wanawake wengine waliozungumza kwenye documentary hiyo, ni waandishi na madensa wake ambao wamesema kuwa alikuwa anawavua nguo zote na kuanza kuwarekodi kwa kamera.

Tayari mwanasheria wa R. Kelly ametangaza kuchukua hatua za kisheria dhidi ya kituo hicho cha Runinga endapo kipindi hicho kitarushwa, kwani wanawake wote waliohojiwa ni waongo na wana lengo la kumchafulia jina R. Kelly .

Documentary hiyo ina sehemu 6 (Episode 1-6) na hapa chini ni episode 1-4 ambazo tayari zimesharushwa mtandaoni na kituo hicho.

Muaandaaji wa Documentary hiyo, Dream Hampton amekanusha taarifa za kuwapanga wanawake hao na ameshangazwa na kitendo cha baadhi ya mastaa kukataa kufanyiwa mahojiano ili watoe maoni yao.

Dream amesema mwanzoni alipata majina 50 ya mastaa kwa ajili ya mahojiano, lakini baadae wote wakakataa kuhojiwa isipokuwa John Legend na Stephanie Edwards.

Mwishoni mwa mwaka 2018, R. Kelly kupitia wimbo wa ‘I Admit’ alikiri wazi kuwa alishawahi kuwanyanyasa mabinti kingono lakini mpaka sasa hajakamatwa wala kuchukuliwa hatua za kisheria.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents