Habari

Wanawake wenzangu tusiogope kuchangia damu -Waziri Ummy

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee ma Watoto, Ummy Mwalimu amewata wanawake nchini kutoogopa kuchangia damu, amewataka kuwa mstari wa mbele katika kuchangia huduma ya damu salama ili kunusuru wakina mama wanaopoteza damu wakati wa kijifungua.

Waziri Ummy ametoa wito huo wilayani Mpanda mkoani Katavi baada ya kutembelea banda la kuchangia damun salama.

“Wanawake Tanzania wanawake wengi wanazana kwamba hawapaswi kuchangia damu kwasababu wanachangia damu kwa njia nyingine lakini wataalam wanatuambia wanawake wanaweza kuchangia damu hadi mara tatu kwa mwaka na wahitaji wakubwa ni wanawake na watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano,” alisema Waziri Ummy.

“Kwahiyo nitoe wito kwa wanawake wenzangu tusiogope kuchangia damu, kuchangia damu ni jambo la kheri lakini pia ni jambo la baraka lakini pia ni ibada kwa mujibu wa dini zetu.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents