Michezo

Wanger afunguka baada ya kutwaa tuzo ‘Tangu nilipoachana na Arsenal nimekuwa nikishinda tuzo kila wiki’

Aliyekuwa meneja wa Arsenal, Arsene Wenger ameonyesha hali ya maskhara hapo jana usiku siku ya Alhamisi baada ya kusema kuwa anajutia kuchelewa kuondoka Arsenal kwasababu sasa anatwaa tuzo kila wiki.

Arsene Wenger was given award by England boss Gareth Southgate on Thursday evening

Mfaransa huyo alitunukiwa tuzo ya ‘lifetime achievement award’ kutoka ‘League Managers Association’ baada ya kutwaa nyingine kama hiyo  ya ‘Leaders Sport Awards’ mapema mwamwezi Oktoba.

Frenchman was handed a lifetime achievement award by the League Managers Association

Meneja wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate ndiye aliyemkabidhi tuzo hiyo mzee Arsene Wenger.

Wenger's 22-year reign in charge of Arsenal came to an emotional end in May this year

Wenger mwenye umri wa miaka 69 amenukuliwa akisema kuwa ”Tangu niachane na kufundisha  nimekuwa nikipata tuzo kila wiki. Huu ujinga gani sikufahamu mapema”

Kwenye usiku huo ambao ulishuhudiwa Wenger akitwaa tuzo hiyo mwenyekiti wa ‘LMA’, Wilkinson amesema Arsene amekuwa na mchango mkubwa sana katika maendeleo ya soka la kimataifa tangu alipowasili kwake Arsenal FC mwaka 1996.

”Ni nafasi yetu kumpa yeye tuzo hii kutokana na kutambua huduma yake iliyotukuka katika maendeleo ya mchezo wa mpira wa miguu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents