Michezo

Wanyama uso kwa uso na msanii wa Bongo fleva anayemkubali (Picha)

Mchezaji wa klabu ya Tottenham Hotspurs ya nchini Uingereza na timu ya Taifa ya Kenya, Victor Wanyama ambaye yupo nchini kwa ajili ya mapumziko mafupi kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu nchini Uingereza August 12 ambapo timu yake ya Tottenham ikiwa ugenini kuvaana na Newcastle.

Victor Wanyama akikabidhiwa CD na msanii  Saida kaloli (kushoto) anaye ipokoea ni Victor Wanyama (kulia) mchezaji wa Tottenham Hutspurs

 

Mara kadhaa katika mahojiano yake na baadhi ya vyombo vya habari nchini, Wanyama amesikika akisema anamkubali mkali wa nyimbo ya O’rugambo ya Saida Kaloli na anapenda sana kufuatilia baadhi ya vibao vya msanii huyo hasa nyimbo hii anayo tamba nayo kwa sasa.

Katika hali isiyo kuwa ya kawaida hatimaye mchezaji huyo kutoka Afrika Mashariki anaecheza ligi kuu nchini Uingereza amekutana na msanii Saida Kaloli na kukabidhiwa CD yenye kibao cha wimbo huo.

Wakati akiwa katika kipini cha Sports Extra kinachorushwa na kituo cha redio cha Clouds FM, Wanyama aliutaja wimbo huo .

“Nafuatilia sana Bongo Flava na wasanii wote wanafanya vizuri kwasasa na nimependa wimbo huu mpya wa ‘O’rugambo’ wa Saida Kaloli.”

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents