Habari

Waombolezaji watoa heshima za mwisho, watumia sekunde 46 muda ambao Floyd alivumilia chini ya goti la polisi

Quincy Mason Floyd ambaye ni mtoto wa marehemu George Floyd Mmarekani mwenye asili ya Afrika aliyefariki dunia mikononi mwa polisi amewashukuru watu wote waliojumuika na familia yao katika kuwafariji kupitia kipindi hiki wanachopitia.

Quincy Mason Floyd (akiwa kati  alipozuru eneo ambalo baba yake mzazi George Floyd aliuawa)

Hayo ameyasema wakati maelfu ya watu wakiwa wamekusanyika katika kutoa heshima zao za mwisho “Ninamshukuru kila mmoja wenu aliyekuja kutufariji wakati huu mgumu wa msiba wa baba yangu.” Quincy Mason Floyd

Waombolezaji waliokusanyika kutoa heshima zao walikaa kimya kwa dakika nane, sekunde 46, muda ambao Floyd alivumilia chini ya goti la polisi mjini Minneapolis hadi akapoteza fahamu.

Duru zinasema kuwa marehemu George Floyd alikuwa na ugonjwa wa Corona . . . ” Si janga la corona lililomuua George Floyd”. ”Janga la ubaguzi wa rangi limemuua Floyd.” Wakili wa familia ya Floyd, bw Benjamin Crump aliwaambia waombolezaji walihudhuria ibada ya kumkumbuka mtu mweusi aliyeuawa tarehe 25 mikononi mwa polisi mzungu aliyechomeka goti kwenye shingo lake.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents