Videos

Waongozaji hawa wanne wa video za muziki Tanzania wanaweza kuziba pengo la Adam Juma?

Habari ya uamuzi wa muongozaji wa video za muziki Tanzania aliyezipeleka Next Level, Adam Juma kuwa ameacha kufanya video za muziki, jana zilipokelewa kwa masikitiko na wadau wengi wa muziki.

Adam Juma na Addo Novemba
Adam Juma

“Kwa kweli pigo kubwa kwa muziki wetu ni mtu ambaye peke yake aliweza kupeleka video za kibongo next level na kutambulika kimataifa sio MTV,Trace, Channel O, very bad kwa kweli I hope atareconsider kurudi kufanya video. He is da best,” alisema msomaji wetu aitwaye Lord Herry.

“Kaamua and I support him,,baadae wasanii ndio watajua pengo lake we subiri utaniambia, Adam kausaidia sana muziki wetu wa leo ila historia yote itakuja kujulikana baadae,” amesema mwanamuziki wa Tanzania aishiye nchini Sweden, Nuru the Light ambaye video zake nyingi zimefanywa na Adama, zikiwemo mpya alizotoa wiki hii za nyimbo zake, Nsuburi Usilale na Wewe.

Ni kweli kabisa pengo la Adam Juma ni kubwa na litachukua muda mrefu sana kuliziba. Hiyo ni kwasababu video nyingi za Tanzania zilizowahi kuchezwa kwenye vituo vikubwa vya runinga duniani ni zile tu zilizotengenezwa na yeye ama waongozaji wa nje ya Tanzania.

Adam ndiye aliyetengeneza video ya Diamond ‘Mbagala’ ambayo ilimsaidia Diamond atajwe kama msanii bora anayechipukia kwenye tuzo za MTV Base zilizofanyika mwaka 2010 jijini Lagos, Nigeria.

Video nyingi za Adam zimewahi kutajwa kuwania tuzo za Channel O, ikiwemo video ya Shaa, Witness, Cpwaa na zingine.

Kwahiyo ni wazi kabisa kuwa kama Adam akishikilia msimamo huo, tutakuwa tumerudi hatua nyingi nyuma na itatuchukua muda kuzikamata tena.

Lakini kuna good news. Wapo vijana wenye uwezo mzuri kwenye fani hiyo ambao kama wakiendelea kukaza huenda wakaweza kuliziba pengo hilo.

Kabla ya kuwataja waongozaji hao watatu, ningependa kusema kuwa wapo waongozaji wengi wa video za muziki nchini wanaofanya kazi nzuri sana na hiyo haimaanishi kuwa hawa wanne bora sana kuwazidi. Lakini kuna vitu ambavyo Adam anavyo na vijana hawa wanaonekana kuwa navyo pia. Wote ni wasomi, wako exposed na wanabadilika haraka kuendana na technolojia mpya katika fani hiyo. Vijana hao ni pamoja na:

Nisher

935618_464553823626182_1656797397_n

Huyu ni director wa video aliyekuja kwa kasi nchini. Kwa muda mfupi sana amekuwa gumzo la nchi. Ni kijana mwenye vipaji vingi sana. Pamoja na kuwa muongozaji na mtayarishaji wa video, Nisher ni mwanamuziki wa rnb, mtayarishaji wa muziki, graphic designer na mambo mengine kibao.

Wiki hii aliweka historia nyingine kwa kufanikisha kuwa na video iliyokubalika kuchezwa kwenye kituo cha Channel O.

Video hiyo ni ya Ben Pol, Jikubali. Pia kuna video ya Feza Kessy ‘Amani ya Moyo’ ambayo naskia nayo imepitishwa.

Niliwahi kuzungumza na Adam Juma na akamsifia sana Nisher huku akidai kuwa kama akiendelea kujituma atafika mbali.

Raqey

48044_10151430489548123_1612975074_n

Raqey ni mpiga picha maarufu zaidi nchini kuliko wote unaowajua. Ni mwanzilishi na CEO wa kampuni ya I-View Studios. Anahusika na utengenezaji wa matangazo mengi ya biashara nchini yanayohusisha graphics na picha. Ndiye mtengenezaji wa makava mengi ya filamu za Tanzania. Kutokana na ubusy alionao kwenye masuala hayo, hukosa muda wa kujikita kwenye utengenezaji wa video lakini ameshawahi kutengeneza video za mbili maarufu ikiwemo Nataka Kulewa ya Diamond na Kwasa Kwasa ya Tazneem.

http://www.youtube.com/watch?v=SzMDns-MgPI

http://www.youtube.com/watch?v=MndS7tFyp4c

Osse Greca Sinare

1013409_563029913747232_2102466719_n

Osse ni mpiga picha pia na amesomea nchini Malaysia. Kuna vitu vingi wanavyofanana na Raqey. Ni mwanzilishi wa OGS Studios ambayo imekuwa ikihusika na kupiga picha za fashion, kutengeneza matangazo na mambo mengine. Osse amewahi kutengeneza video ya One The Incredible ‘Got Em’.

Mara ya mwisho nimekutana naye aliniambia kuwa kuna mzigo wa vifaa vya kisasa unakuja na huenda akaanza kufavya video za muziki zaidi.

Henry M (Hefemi Studios)

Sijawahi kukutana na Henry lakini nafahamu kuwa anaishi nchini Marekani. Fani yake halisi ni udaktari lakini utengenezaji wa video ni kitu anachokifanya kama hobby lakini anakiweza sana. Ametengeneza video ya kundi la kinadada la Shosteez, On the Floor.

http://www.youtube.com/watch?v=Q8Femv2IvWw

Hivi karibuni alikuja nyumbani Tanzania kuchukua jiko (kuoa). Hata hivyo Henry amekuwa akifanya zaidi video za wasanii wa nchi zingine kama Nigeria nk.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents