Habari

Wapakistani wahukumiwa kurudi kwao na kulipa faini kwa kuihujumu TCRA

Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam,imetoa hukumu ya kurejeshwa kwa raia watatu wa Pakistani waliokuwa wakiishi hapa nchini kufuatia kupatikana kwa makosa mbalimbali ikiwemo kosa la kuhujumu mitambo ya mawasiliano ya kimataifa na kuisababishia serikali hasara ya mamilioni ya fedha kupitia mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA).

screen-shot-2016-11-02-at-5-05-53-pm

Raia hao, Hafees Irfan, Mirza Irfan Baig na Mirza Rizwani Baig, mnamo Oktoba 15 mwaka jana, wakiwa katika hoteli ya Butterfly iliyopo Kariakoo, jijini Dar es salaam walifanya kosa hilo kwa kutumia vifaa maalumu vya mawasiliano vilivyotumika kupiga simu za kimataifa pasipo kibali maalum cha mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA huku watuhumiwa hao wakikiri kufanya makosa hayo.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu mkazi wa mahakama ya Kisutu, Respicious Mwijage amesema kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wahusika hao watalazimika kutoa faini ya shilingi milioni 40 kwa kila mmoja au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela sanjari kurejea nchini kwao maramoja watakapo lkamilisha ulipaji wa faini hizo.

Akizungumzia hukumu hiyo Mwanasheria wa Mamlaka ya mawasiliano Nchini TCRA, Johanne Kalungura, ameeleza kuridhishwa na adhabu iliyotolewa na Mahakama na kuongeza kuwa itakuwa fundisho kwa wenye nia ovu ya kuhujumu Uchumi wa nchi.

“Kwahiyo mahakama imetoa amri walipe hizo pesa halafu vilevile vifaa vyote vya mawasiliano vimetaifishwa kuwa mali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania,vilevile mahakama imetoa amri hawa watu wafukuzwe nchini mara moja kwahiyo watuhumiwa hao wamekamatwa watapelekwa idara ya uhamiaji na wanapaswa waondoke nchini,”alisema Kalungura.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents