Burudani ya Michezo Live

Wapambe wa Bobi Wine waonywa kupiga kampeni kwa kuandika na kuzichafua fedha za Uganda

Wapambe wa Bobi Wine waonywa kupiga kampeni kwa kuandika na kuzichafua fedha za Uganda

Raia wa Uganda wamekuwa wakiandika jumbe za kisiasa kwenye noti za fedha, ambapo jumbe nyingi ni za kushawishi kuchaguliwa kwa Mbunge Bobi Wine kuwa Rais katika uchaguzi wa 2021.

Benki Kuu ya Uganda imesema vitendo hivyo ni uhalifu na vianaashiria ukosefu wa maadili. Aidha benki hiyo imefafanua kwamba kwa kuandika maneno kwenye fedha, kunaashusha thamani yake, na kuharibu ubora na ulinzi wake.Kwa kweli hii inaweka Hali ya wasi wasi kwa maneno ambayo yameandikwa au kuchafuliwa kwa njia yoyote.”Benki imebaini kuhusu wasiwasi kwa habari kadhaa zianazovuma kwenye mitandao ya kijamii zinazozunguka picha za sarafu za Uganda zikiwa na ujumbe wa kampeni za kisiasa.

Hii ni kushauri wananchi wote kuwa makini, kuandika alama kwenye noti au sarafu huingiliana na huduma za usalama.

 

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW