Habari

Wapinzani wanaotoa kauli za kichochezi kushtakiwa kwa makosa ya uhaini

Bunge la Katiba nchini Venezuela limepiga kura kwa kauli moja kuunga mkono viongozi wa upinzani kushtakiwa kwa makosa ya uhaini, endapo watatoa kauli za kichochezi nchini humo.

Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro.

Maamuzi hayo ya bunge yamekuja kwa shinikizo kubwa kutoka kwa Rais wa nchi hiyo, Nicolas Maduro baada ya viongozi wa upinzani kuishinikiza Marekani kuiwekea vikwazo vya kiuchumi nchi hiyo baada ya mauaji ya magenge ya wauza unga nchini humo kutekelezwa bila kufuata sheria.

Rais Maduro mara kwa mara amekuwa akiwatuhumu viongozi wa upinzani kuwa wanaushirikiano mkubwa na Marekani, nchi ambayo anadai inaufedhuri na inajiandaa kwa uvamizi wa kijeshi nchini humo.

SOMA ZAIDI – Wananchi wa Venezuela wamkalia kooni Rais Nicolas Maduro

Hata hivyo wiki iliyopita Rais wa Marekani, Donald Trump aliitangazia vikwazo vya kiuchumi Venezuela huku akimuonya Rais Maduro kuwa kama ataendelea na vitendo vya ukiukaji wa haki za kibinadamu ataingilia kati kwa uvamizi wa kijeshi nchini humo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents