Siasa

Waporaji Benki Kuu wafilisiwe – CCM

Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imetaka wote watakaobainika kuhusika katika upotevu wa fedha Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wafilisiwe mali zao zote ili kufidia fedha hizo.

Na Theodos Mgomba, Dodoma

 
Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imetaka wote watakaobainika kuhusika katika upotevu wa fedha Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wafilisiwe mali zao zote ili kufidia fedha hizo.

 

Aidha kamati hiyo, imesema hatua hiyo inatakiwa kutekelezwa sambamba na hatua zingine za kisheria na kinidhamu dhidi yao.

 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari mjini hapa juzi na Katibu Uenezi wa chama hicho, Bw. John Chiligati, hatua ya kuwafilisi mali zao itasaidia kurejesha fedha za umma.

 

Alisema hatua hiyo ikichukuliwa itakuwa ni fundisho kwa wengine ambao wana tabia ya kuchezea fedha za umma.
Kwa upande mwingine alisema Kamati Kuu imeiagiza serikali kutoa taarifa ya mara kwa mara ya kamati iliyoundwa kuchunguza upotevu huo wa fedha kwa wananchi.

 

Alisema utoaji wa taarifa ya hatua mbalimbali zinazofikiwa na kamati hiyo itawezesha wananchi kujua imefikia wapi badala ya kukaa bila kujua kinachoendelea ndani ya kamati hiyo.

 

Aidha kamati hiyo imempongeza Rais Jakaya Kikwete na serikali yake kwa hatua alizozichukua dhidi ya upotevu huo katika kupambana na ufisadi.

 

Chiligati alisema hatua ya kuchunguza benki hiyo si hoja ya wapinzani kama wananchi wengi wanavyoelewa hivi sasa bali ilishatolewa na Rais Kikwete mapema mwaka jana.

 

Hatua ya kutaka BoT hasa akaunti hiyo ya nje kuchunguzwa ilitolewa na Rais siku nyingi na kazi ya kutafuta kampuni binafsi ilianza na si wapinzani walioanzisha mchakato mzima wa suala hilo kama inavyoeleweka hivi sasa, alisisitiza.

 

Source: Nipashe

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents