Soka saa 24!

Wasanii wajipanga kuwafuta machozi waathirika wa Mv Spice Islanders

Fa_na_ay
Mwenyekiti wa chama cha wasanii wa muziki wa Bongo Fleva Mwana Fa amesema wasanii wamekubali kwenda kufanya show, ya bule ili kuchangia katika mfuko wa watu walioathirika katika ajali ya Mv Spice Islanders iliyozama maeneo ya Nungwi wakati ikitoka Zanzibar kwenda Pemba wiki iliyopita.

Mwana Fa amesema kwa sasa wanajitahidi kushughulikia sula la kupata fedha, kwaajili ya maladhi na chakula kwaajili ya wasanii walio jitolea kwenda huko.  amesema anatarajia kwenda na wasanii wapatao kama kumi, ambao kwa pamoja wataungana na wasanii wa Zanzabar na kufanya Show ya pamoja tarehe 24, ilikuweza kupata fedha kwaajili ya kuchangia watu waliopata maafa ya ajali hiyo.

Miongoni mwa watu ambao wanatarajia kwenda huko ni Mkubwa na Wanawe Band asmbayo inaongozwa na Fella, ambaye amesema yeye kajitolea na bendi yake.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW