Warembo 30 waingia kambini kujiandaa na Miss Redd’s Tanzania

Warembo 30 kutoka sehemu mbalimbali nchini wameingia kambini jana kwenye hoteli ya Giraffe kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kushiriki shindano la Redd’s Miss Tanzania 2012 litakalofanyika Novemba 3 Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jana Mkurugenzi wa kampuni ya Lino Agency International , Hashimu Lundenga alisema kuwa warembo wote walishapewa taarifa za kuripoti kambini jana na mara baada ya kuwasili watapewa taratibu za kambi hiyo.

Lundenga aliwataka washiriki hao kuhakikisha wanawasili asubuhi na mapema katika ofisi za kamati ya Miss Tanzania kama walivyoambiwa ili wapelekwe pamoja katika hoteli hiyo iliyoandaliwa kwa ajili ya kambi yao ya mwezi mzima.

Alisema warembo hao wakiwa katika kambi ya Redd’s Miss Tanzania watafundishwa mambo mengine muhimu katika maisha yao ambayo yatawafanya wajiandae kuwa wanawake walio na maendeleo na watakaokuwa tayari kuongoza familia zao.

Alisema pia baada ya kumpata mshindi atakapewa mapumziko ya miezi miwili na baadaye ataanza maandalizi ya kujiandaa kuiwakilisha nchi katika mashindano ya dunia ya mwakani.

Alisema kuwa licha ya kuwepo na changamoto mbalimbali katika mashindano hayo, anawapongeza mawakala kwa kazi ya kusaka warembo ambao wengi wao walifanikiwa kufuzu fainali hizo ni wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents