Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Warembo sita wajitokeza Miss Upanga

Warembo sita wamejitokeza kushiriki katika shindano la kumsaka mrembo wa kitongoji cha Upanga, Miss Upanga 2006 ambalo limepangwa kufanyika Mei 20 jijini Dar es Salaam.

2006-03-20 10:04:48
By Chile Kasoga

Warembo sita wamejitokeza kushiriki katika shindano la kumsaka mrembo wa kitongoji cha Upanga, Miss Upanga 2006 ambalo limepangwa kufanyika Mei 20 jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa mashindano hayo, Malick Fundikira kutoka kampuni ya Smilling Face, alisema kuwa fomu kwa ajili ya wanaotaka kushiriki shindano hilo bado zinaendelea kutolewa huku akiongeza kuwa mazoezi yameshaanza kwenye ukumbi wa Latavena.

Fundikira alisema fomu hizo zinapatikana katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam na kutoa wito kwa wasichana wanaopenda kushiriki kujitokeza kwa wingi kabla ya Aprili 30.

Alizitaja baadhi ya maeneo zinapopatikana fomu hizo kuwa ni Millenium Tower na Plaza photo point Maethea.

Aliwataja washiriki hao waliojiandikisha mpaka sasa kuwa ni Magreth, Sabrina, Khadija, Judith na Zainab na Helen.

Fundikira alisema mpaka sasa makampuni kadhaa amejitokeza kutaka kudhamini shindano lao na kuwataja kuwa ni Redds Premium Cold, CxC Holdings pamoja na Computer Solution na kutoa wito kwa makampuni mengine kujitokeza kudhamini shindano hilo.

  • SOURCE: Nipashe

{mos_sb_discuss:10}

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW