Warembo wafungiwa milango MMB na Madee

Msanii wa muziki Bongo, Madee amesema hana mpango wa kumsimamia msanii yeyote wa kike katika label yake ya Manzese Music Baby (MMB).

Madee amesema sababu ya kufanya hivyo ni ili kuepukana na usumbufu ambao anaweza kuupata.

“Hapana, sipendi tu mambo hayo namwachia Daxo Chali, ndio anayaweza. Siwezi tu kukaa na watoto wa kike kwa sababu jinsia tofauti tutapishana maneno ataona nimemuonea,” Madee ameiambia Clouds FM.

Madee ameongeza kuwa kila siku hupokea simu zaidi ya 20 za wasanii wakitaka usimamizi chini ya MMB lakini kutokana hawezi kuwasaidia wote huishia kuwashauri. MMB kwa sasa ina wasanii wawili ambao ni Dogo Janja na Gaza.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW