Michezo

Warriors waandaa kitita cha fedha kumnasa LeBron James wa Cavaliers

Staa wa mchezo wa mpira wa kikapu nchini Marekani anayekipiga katika timu ya Cleveland Cavaliers, LeBron James huwenda mwishoni mwa msimu akasajiliwa na Golden State Warriors kwa dau nono litakaloweka rekodi ya ligi ya NBA.

Tayari Warriors wameonyesha nia ya kuhitaji huduma  ya staa huyo kwa kumtengea kitita cha pauni milioni 95 kiasi ambacho kinaelezwa kuwa ni kikubwa kuwahi kutokea katika ligi hiyo.

Mpaka sasa mchezaji huyo bora mara nne  hajaonyesha nia ya kuondoka akihitaji Warriors kufungua milango zaidi ya mazungumzo.

Kwa mujibu wa shirika la ESPN, Golden State ipo tayari kutoa kiasi hicho cha fedha pamoja na kuzungumzia kiasi cha posho kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 33.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents