Burudani

Wasafi TV na Wasafi Redio kuanza kwenda hewani February – WCB

Baada ya kusambaa video mtandaoni inayoonyesha mjengo mpya wa WCB ambao utatumika kama makao makuu ya kampuni hiyo pamoja na studio za Wasafi TV na Wasafi Redio, Meneja wa WCB amefunguka kulizungumzia hilo.

Akiongea na Gazeti la Mwananchi, Mkubwa Fela amesema hatua waliofikia ni katika harakati za kampuni hiyo kuendelea kujitanua na kutoa fursa kwa vijana wengi.

Fela amesema pamoja na kwamba wao ni watu wanaojishughulisha na kazi za burudani, lakini TV yao na redio zitakuwa zinarusha vipindi vya aina zote vikiwemo vya kuelimisha na habari kama vilivyo vituo vingine.

“Kwetu sisi hii tunaona ni hatua nzuri kwa kuwa tunajua tukifungua vituo hivi ndivyo kadri tunavyozidi kuzalisha ajira na tumeamua kutumia wataalam ambao walikuwa kwenye fani hiyo ikiwemo wazee waliostaafu katika Shirika la Utangazaji(TBC) enzi hizo TVT kwa ajili ya kutuongoza kwa kuwa sisi wenyewe hatuwezi,”amesema Fela.

Hata hivyo, alipoulizwa kama wamejenga wenyewe mjengo huo au Fela amesema wamekodisha kama walivyokuwa wamekodisha ile ya Sinza huku sababu za kuhama akieleza ni kutokana na kuongeza huduma na pia sehemu waliyokuwepo kulikuwa na taabu ya maegesho ya magari na kujaa maji hasa mvua zinaponyesha.

Mjengo huo wa wasafi wa ghorofa moja ambao upo maeneo ya Mbezi umeonekana kuwa gumzo leo Alhamisi katika mitandao ya kijamii na watu wengi wamempongeza Diomond na uongozi wake kwa hatua aliofikia.

Mbali na redio, tayari Diamond ameshajiingiza katika biashara nyingine ikiwemo ya manukato yanayoitwa ‘Chibu’, na ‘Diamond karanga’

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents