Habari

Wasafiri watoa maoni yao kuhusiana na usafiri wa treni jijini Dar es Salaam


Baada ya wizara ya uchukuzi kufungua rasmi usafiri wa treni jijini Dar es Salaam, baadhi ya wananchi wameongea na bongo5 katika kituo cha Ubungo na kutoa maoni yao huku wengi wa wasafiiri wakimpongeza Dk Harrison Mwakyembe.

Wamesema hatua hiyo ni kubwa ya kihistoria na halikutegemewa kutokea siku za usoni, kwasababu mradi huo ulikuwepo toka muongo mmoja uliopita.

Wamesema usafiri huo utakuwa chachu kwa maendeleo kwa sababu foleni ya magari itakuwa kwa kiasi na hivyo watu watafanya kazi masaa mengi bila kufikiria swala la usafiri.
Aidha wamesema nauli ambayo ni shilingi 400 kwa mtu mzima na shilingi 100 kwa wanafunzi ni bei nzuri inayoendana na uchumi wa watanzania wengi.

Hata hivyo wameongeza kuwa kunahitajika maboresho kuanzia kwenye ukataji tiketi na sehemu za kupumzikia wakati wakisubiri usafiri huo.

Wameulalamikia mfumo wa ukataji wa tiketi kuwa sio mzuri ambao unasababisha msongamano mkubwa huku wengine wakilalamikia kusubiri kwa muda mrefu.

Abiria wa usafiri wa treni wakikata tiketi Ubungo

Wametoa ushauri kwa mamlaka husika kuweka ratiba makini ya treni kwa kila kituo ili abiria wajue muda gani watapanda.

Kingine ni pamoja na kuongeza idadi ya mabehewa kwa kila treni kwakuwa wamesema wamekuwa wakibanana kiasi cha kuweza kuhatarisha afya zao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents