Bongo5 Makala

Wasanii 10 wapya wa Tanzania wa kuwaangalia mwaka 2014

Mwaka 2014 huu hapa. Unatuahidi mazuri kwenye burudani kuliko mwaka 2013? Ni mapema kujua hilo hivyo ni bora kusubiri. Mwaka jana tulitoa orodha kama hii ambapo miongoni mwa tuliowaweka ni pamoja na Young Killer, Vanessa Mdee, Ally Nipishe ambao tunafurahi kuona kuwa kweli walifanya vizuri nab ado wanaendelea kujidhatiti. Hawa ni wasanii wapya 10 wa kuwaangalia mwaka 2014.

Nuh Mziwanda

Nuh Mziwanda

Jina la Nuh Mziwanda linaweza lisiwe geni sana kwenye masikio ya wengi kwakuwa wimbo wake wa mwaka jana, Otea Nani ulifanikiwa kupata airtime kwenye vituo vingi vya radio nchini. Video ya wimbo huu imetoka jana, (Jan 1,2014) na hivyo video inaweza kumsogeza mbele zaidi na hakuna shaka kuwa jina lake litasikika sana kwenye baadhi ya show za mjini. Nuh ni msanii sampuli ya Diamond, Richie Mavoko na waimbaji wengine wa Bongo Flava pendwa.

Baraka

baraka

Baraka ni msanii kutoka Mwanza ambaye jina lake huko si geni kwenye mitaa ya jiji hilo la Mawe. Akiwa Mwanza, pamoja na kufanya nyimbo kadhaa zake mwenyewe, Baraka amewahi kushirikishwa kwenye nyimbo kadhaa za wasanii wa Mwanza. Mwaka jana alihamia Dar es Salaam na kufanya nyimbo kadhaa na Bob Junior ambazo hata hivyo hazijatoka. Akiwa chini ya uongozi mpya utakaojulikana rasmi hivi karibuni, Baraka amesharekodi zaidi ya nyimbo 3 na atafanya video ya kutambulisha rasmi wimbo wake wa kwanza mapema mwaka huu.

Ayler Ayrine

ayler

Irene Peter aka Ayler ni msanii kutoka Arusha aliyesoma kwenye chuo cha usimamizi wa fedha, IFM. Tayari ana video yake ya wimbo uitwao Msamaha na pia ameshirikishwa kwenye wimbo wa rapper wa Arusha, Gentriez uitwao, Bembeleza.

Hisia
IMG_9764

Elisha Hisia alikamata nafasi ya 4 kwenye shindano la Tusker Project Fame msimu wa 6 na uwezo wake unaonesha kuwa atakuwa msanii mkubwa si tu Tanzania, bali Afrika Mashariki kwa ujumla. Tayati ana wimbo mpya aliourekodi wakati wa shindano hilo uitwao Just For You (Kwaajili Yako).

[soundcloud url=”https://api.soundcloud.com/tracks/125435700″ params=”color=ff6600&auto_play=false&show_artwork=true” width=”100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Angel

Angel

Angella Karashani ni mwakilishi mwingine wa Tanzania kwenye TPF6. Kabla ya kushiriki shindano hilo, tayari sauti yake ilishasikika kwenye wimbo wa Ommy Dimpoz, Baadaye na mwaka jana alitajwa kuwania tuzo za KTMA kwenye kipengele cha msanii bora mpya. Mwishoni mwa mwaka 2013 aliachia wimbo mpya uitwao Maumivu.

Asia

Asia

Asia ni msanii wa THT ambaye hadi sasa ana nyimbo mbili, Mtoto wa Mjini na Nawaumbua aliomshirikisha Shilole. Ni msanii wa mduara ambaye hadi sasa ameshapanda steji moja na wasanii wakubwa wa aina ya muziki anaofanya. Mwaka 2014 anaweza kufanya vizuri zaidi.

http://www.youtube.com/watch?v=Iu_b_YN_1VY

PBling

P-Bling

Jina la P-Bling aka Yung Shark, linaweza kuwa geni kabisa kwenye masikio yako na huenda hujawahi kusikia wimbo wowote ule kutoka kwake. Ni rapper ambaye kwa muda mrefu amekuwa karibu sana na producer wa De Fatality, Mesen Selekta.

Si rapper wa kawaida, ni rapper mkali ambaye kama ukimsikia kwa mara ya kwanza wazo la kuwa anaweza kuwa ni Mtanzania linaweza lisipite kabisa kwenye akili yako. Ni rapper kibonge hivi, ambaye kama angekuwa na ndevu kama Rick Ross, basi ungedhani wana undugu. Uwezo wake naufananisha na Drake hasa ule ujuzi wa kurap vizuri na kuimba sauti tamu za chorus kama afanyavyo Drizzy.

Nyimbo zake nyingi zimekuwa za mixtape zaidi ambapo tayari ameshafanya mixtape ikiwemo ile iitwayo ‘Just Because: The Mixtape’. Ameshafanya nyimbo kama Black on Black, Turn My Music Up, Dropping Them Bombs, Where You Haters At na zingine.

Lakini nakuhakikisha kuwa, ukimpa muda na sikio lako, unaweza kuwasahau rappers wengi wa aina yake unaowafahamu.Ili kujua uwezo wake, sikiliza/tazama cover hii aliyoifanya kutumia wimbo wa Dj Khaled ‘I’m on One’ ambayo yeye ameiita ‘Nothing to Me’.

http://youtu.be/5vnZ5LRv2Ew

Damian Soul
bd6d1d70527411e38ef91257c578f500_7

Damian Soul alishiriki shindano la Tusker Project Fame msimu wa 5 japo alitoka mapema. Hata hivyo msanii huyo wa soul alikuja kuwathibitishia watu kuwa majaji wa TPF hawakukiona kipaji chake baada ya kuanza kushiriki kwenye matamasha makubwa ikiwa pamoja na Sauti za Busara mwaka jana ambapo alimsindikiza Peter Msechu. Mwaka jana alishirikishwa kwenye wimbo wa Lord Eyez, Mapito na pia kuachia wimbo wake, Mpenzi aliomshirikisha Joh Makini.

Mike (Michael Lukindo)

1239516_423891174398213_1134488285_n

Mike ni mtangazaji wa East Africa Radio kutoka Arusha. Ni miongoni mwa watangazaji wabunifu kwenye kituo hicho. Pamoja na utangazaji, Mike ni muimbaji mzuri wa R&B ambaye uwezo wake umeshangaza wengi baada ya kuachia wimbo Likizo aliomshirikisha Joh Makini na Damian Soul.

[soundcloud url=”https://api.soundcloud.com/tracks/122577988″ params=”color=ff6600&auto_play=false&show_artwork=true” width=”100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Kadja

kadja

Kadja ni msanii mwingine wa THT anayestahili kuangaliwa zaidi mwaka 2014. Ni msanii mwenye uimbaji kama Linah na mwaka jana aliachia video ya wimbo wake, Maumivu.

http://www.youtube.com/watch?v=cwIEP9NHSYg

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents