BurudaniUncategorized

Wasanii 8 wa Bongo Flava wanaomkosha Rama Dee

Msanii wa RnB Bongo, Rama Dee ametaja list ya wasanii anaowakubali kutoka kwenye Bongo Flava.

Muimbaji huyo ameiambia EA Radio kuwa yeye anapenda kuchanganya makundi yote katika muziki bila kujali ni aina gani ya muziki msanii husika anafanya ila anachoangalia ni yupi ambaye anamburudisha zaidi.

“Nawakubali artist wengi sana, kwa mfano nawakubali Weusi, Fid Q, ana uwezo mkubwa sana naweza kusema, mwingine ni Banana Zoro, Peter Msechu, Barnaba ni watu unique ukisikia sauti hai-sound sehemu nyingine ndio kitu ambacho na appreciate. Pia Lady Jaydee, Joh Makini ni mtu ambaye ukisikia sauti yake ni fresh,” amesema Rama Dee.

Hitmaker huyo wa Kuwa na Subira, Kama Huwezi na Kipenda Roho kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Nibebe’.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents