Burudani

Wasanii hawana ueledi kwenye Bongo Fleva – SSK

Kundi jipya la muziki wa Hip Hop Bongo, Sisi Sio Kundi (SSK) wamebainisha kuwa wasanii kutofanya kazi kwa ueledi ni moja ya sababu ya vitu ambavyo hawavipendi kwenye game.

Kundi la SSK (Wakazi, Zaiidi, P the MC na Cjamoker

Member wa kundi hilo,Wakazi, amesema watu kutokuwa professional, kutokujua na kuthamini kazi wanayofanya ni miongoni mwa vitu asivyopendezwa navyo kwani muziki unapaswa kuchukuliwa kama ajira.

“Muziki ni kama umejiajiri lakini wabongo wanachukulia kama umejiajiri inabidi uamke saa sita (mchana) au muda unaotaka wewe, mtu ukijiajiri unatakiwa uwe makini zaidi kuisimamia kazi unayoifanya kwa sababu kila kitu ni mzigo wako mwenyewe.

“Unapoichukulia hii kama kazi au biashara na mtaji, utafika mbali, mimi sipendi vitu vinavyofanyika unprofessional ndio maana hata kimataifa hatufanyi vizuri,” amesema Wakazi.

Kwa upande wake, P the Mc amesema kwa hapa Bongo, imefikia wakati watu wakiona fulani amefanya kitu na unajua kitakuwa kikali wanatafuta namna ya kukificha na kukizima ilimradi kisikifikiwe, kitu ambacho hakipendi bali anahitaji wasanii kusaidiana.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents