BurudaniVideos

Wasanii 50 wakamilisha video ya miaka 50 ya amani

50_YA_UHURU_FACE
Wasanii50 wa muziki wa kizazi  wamekamilisha video ya maalum ya kuadhimisha miaka 50 ya amani, kwa kuimba wimbo wa pamoja katika viwanja vya taifa  katika kuadhimisha miaka 50 ya amani nchini. Akizungumza na mwandishi wa safu hii, kiongozi wa kundi la Tmk Wanaume Saidi Fella ‘Mkubwa Fella’ amesema lengo la wasanii ni kuwakumbusha Watanzania kwamba miaka 50 na chaguzi nyingi zimepita ni jambo la kujipongeza.

 

WASANII_MIAKA_50

Wasanii 50 na wadau mbalimbali  waliudhulia tamasha hilo la video na  waziri wa michezo, wakiwemo wanamitindo , Miongoni mwa wasanii  waliokuwemo ni Joseph Haule ‘Prof J’,  Amani Temba ‘Mh Temba’, Abwene Yesaya ‘Ay’, Mwijuma Hamisi ‘Mwana Fa’, Abdull Syskes ‘Dully Syskes’, Estarina Sanga ‘Linah’ na Madee.

“Ni wimbo ambao tunashukuru kwa watanzania kudumisha amani miaka yote hiyo, pia tunakumbushana kwamba amani ni jambo la muhimu sana” alisema Mkubwa Fella.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents