Habari

Wasanii kwenye Sauti za Busara

Richard

Wakati tamasha la Sauti za Busara, wasanii mbali mbali walinaswa katika kamera ya B5 wakishuhudia yaliyokuwa yanajiri katika eneo hilo huku baadhi ya wasanii hao wakitoa ushauri na mitazamo yao juu ya tamasha hilo.


Tulikutana na Richard wa Big Brother, aliteta kidogo na Bongo5 na  kusema, ‘Inafika wakati Watazania hususan wasanii waache ulimbukeni wa kutotembea sehemu za matamasha kwa kisingizo hawakualikwa. Matamasha makubwa kama haya, yana ‘Advantage’ kubwa, kwani wasanii wanajifunza mengi sana kutokana na kuyashuhudia yanayojiri.’

 

Aliwaomba wadau waweze kudhamini matamasha hayo, na kuwataka wafadhili na wadhamini wanaiozunguka maeneo hayo waweke kiwango kidogo cha malipo kuanzia Hotelini mpaka kiingilio kusudi kiwavute Watanzania wengi sana waweze kuja, kwani watu wanashindwa kuja kutokana na bei kali za malazi.

Ibra
Kamera ya Bongo5, ilimnasa Ibrahim Mwanza aka Ibra De Husla toka kwenye kundi la muziki wa kizazi kipya Nako2Nako lililojichimbia pande za Arusha, yeye alisema tamasha la Sauti za Busara ni ‘Perfecto’ akiongea kifaransa, huku akifafanua kwa kusema tamasha hilo, linamfanya msanii awe na Experience, Hard Work, na kumfanya aujue zaidi muziki wa kimataifa.

Sauda

Huyu ni mwanamuziki Sauda ambaye alikuwa miongoni mwa wasanii waliopanda jukwaani siku ya Jumatano kuiwakilisha Tanzania kwenye tamasha hilo, Sauda aliiomba uongozi uweze kupunguza kiingilio ili watanzania wengi waweze kuhuhuria, ‘Watu wanashindwa kuja kutokana na usafiri mkubwa, bei za mahoteli na kiingilio,’ alisema Sauda

Kanga

Farouque Abdela, mbunifu wa mavazi ya khanga alisikika akitoa pongezi kwa waandaaji wa tamasha,

Mzungu_Kichaa

Pia nilikutana na Mzungu kichaa, ambaye alionyesha furaha sana kwenye tamasha hilo,

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents