Tupo Nawe

Wasanii maarufu Ghana, Stonebwoy na Shatta Wale wanyang’anywa tuzo kubwa nchini humo kwa kushikiana Bastola jukwaani

Wasanii maarufu nchini Ghana, Shatta Wale na Stonebwoy wamenyang’anywa tuzo za muziki za Vodafone nchini Ghana kwa kosa la kusababisha vurugu na uvunjifuwa amani.

Image result for stonebwoy vs shatta wale
Shatta Wale na Stonebwoy

Waandaaji wa tuzo hizo za Vodafone, wamedai kuwa wasanii hao wawili Shatta Wale na Stoneboy Jumamosi ya wikiendi iliyopita walileta vurugu kwenye ukumbi hadi wakafikia kutoleana bastola.

Tukio hilo lilitokea baada ya Stoneboy kushinda tuzo ya Msanii bora wa mwaka wa Reggae/Dancehall, Jambo ambalo lilimfanya Shatta Wale kunyanyuka na mabaunsa wake na kupanda jukwaani akimfuata na kumpigia makofi kwa ushindi huo.

Stonebwoy yeye alipoona kundi la mpinzani wake mkubwa nchini humo likimfuata, Aliamua kutoa bastola huku akiwataka wasimsogelee tukio ambalo lilizua taharuki kwenye ukumbi wa kimataifa wa AICC.

Hata hivyo, baada ya tukio hilo. Stonebwoy amesema kuwa alitoa bastola kwa lengo la kujilinda kwani hakujua kwanini? mpinzani wake amenyanyuka na kundi la watu kwenda kumpongeza.

Tayari Stoneboy ameshaomba msamaha kufuatia tukio hilo, lakini uongozi wa tuzo hizo umemnyang’anya tuzo mbili alizoshinda kwenye tukio hilo.

I am really sorry for the incident that happened earlier on and I only had to react out of natural instincts because we all know how premeditative some people can be. We have seen on social media the treats and everything so we couldn’t come in unprepared because anything could have happened like you guys saw,” .

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW