Burudani

Wasanii nyota Mejja aka Okwonko na Dogo Richie waingia studio kufanya kazi mpya

Msanii Mejja a.k.a Okwonko anaefahamika kwa sana Africa kwa kibao chake “Utawezana” alichoshirikishwa na Femi One, anaonekana kuto legeza kamba ya kufanya collabo na wasanii nyota nchini Kenya. Akiongea na muandishi wa Bongo5 nchini Kenya Changez Ndzai, Mejja amefunguka baada ya kipost picha kwenye mtandao wake wakijamii akiwa studio na msanii staa Dogo Richie.

“Ni kweli tumeingia studio kwa produza Vicky Pondy ili kufanya kitu kipya na Dogo Richie, yeye ni staa mkubwa kwasasa na anaheshima ya hali ya juu kupitia muziki. Ni wengi wanatamani kupata fursa hii, kwa hivyo japo Mimi nina nafasi yangu katika soko la muziki naona tukishikana pamoja tunaweza fika mbali.” Alimalizia Mejja.

Mejja anakua mmoja ya wasanii ambao wametengeza collabo nyingi zaidi mwaka huu wa 2020, huku Dogo Richie akiwa anasifika kwa kuwashika mkono wasanii wachanga nchini Kenya kupitia wakfu wake wa RICLAM.

Imeandikwa na muandishi Changez Ndzai- Kenya

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents