DStv Inogilee!

Wasanii tunafeli kwa sababu ya ujanja janja wetu, hii ni zama ya JPM tutaumia – Barakah The Prince

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Barakah The Prince amedai kuwa wasanii wengi nchini wanafeli kwa sababu ya kutotii sheria za serikali hasa hasa kanuni za BASATA ambao ndio walezi wake.

Akiongea na Bongo5 amesema kuwa wasanii wengi wanalalamika kuhusu tozo na kodi wanazochajiwa wanapotoka nje ya nchi kufanya show, jambo ambalo lipo wazi tangu zamani ingawaje awali walikuwa wanafanya show nje ya nchi kimya kimya.

Barakah amedai pia yeye ni mtu ambaye anafanya kazi ya muziki kwa kufuata sheria za serikali na ndio maana haijawahi na haitatokea kufungiwa nyimbo zake kama ilivyo kwa wasanii wengine.

 

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW