AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Wasanii tunaingiza hela lazima tulipe kodi, tusiwaonee BASATA wanasimamia sheria – Barakah The Prince (+video)

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Barakah The Prince amesema kuwa wasanii nchini waache kulalamika kuhusiana na malipo ya kibali cha kutoka nje wakati wanaenda kuperform kwani malipo hayo yanawasaidia BASATA kuweza kuendesha baadhi ya kazi zao ambazo zitaisaidia sanaa yetu.

Barakah amesema ili sanaa yetu ikue ni lazima wasanii waende sawa na sheria ikiwemo kulipa kodi na kudai kuwa kulipia kibali hiyo ni sheria ambayo ipo karibia kila nchi ingawaje wasanii wengi walikuwa wamezoea janja janja kipindi cha nyuma.

Akikoleza hoja yake amesema kuwa kitendo cha kulipia ada BASATA zitawafanya wasanii waheshimike na kuwa na sauti ya kusikilizwa na kutatuliwa matatizo yao.

Related Articles

13 Comments

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW