Burudani

Wasanii wa filamu Bongo warudi shule-Ezra

Msanii chipukizi katika filamu nchini, Ezra Makala amewataka wasanii wa filamu nchini kurudi shule ili waweze kufika katika nyanja za kimataif, licha ya kuwa hakuna msanii anaemkubali bongo.


Ezra Makala

Akiongea na Bongo5, amesema kuwa wasanii wengi bongo hawana elimu katika sanaa na ndio maana amekuja kuleta mapinduzi katika tasnia hiyo ya filamu nchini. Pia amewataka wasanii kurudi shule kujifunza mambo ya kisanii kama wanataka kufika viwango vya kimataifa.

Ezara pia ameeleza kuwa hapa bongo hakuna msanii anayemuangalia kama role model Wake isipokua marehemu Kanumba pekee ndio alikuwa akimuangalia.”Nimeacha kuangalia movie za Tanzania kwa kuwa baadhi ya filamu bongo zinaiga kutoka Nigeria, na pia hakuna mabadiliko ya waigizaji ndio maana hakuna ladha katika filamu” alisema Ezra.

Muigizaji huyo amewataka watu kukaa mkao wa kula kwakua anakuja na filamu yake mpya, ‘FATHER Ezra (The Hidden Agenda)’ hivi karibuni.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents