Bongo Movie

Wasanii wa filamu Tanzania waaswa kutumia lugha ya kiswahili

Aliyekuwa Director wa ZIFF Professor  Martin Msando amewaasa wasanii wa filamu Tanzania kutumia lugha ya kiswahili katika kazi zao za sanaa.

Professor Msando ameyasema hayo leo Dar es Salaam katika kikao walichofanya na wasanii wa filamu na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe. Professor Msando aliwasii wasanii hao kutumia lugha ya kiswahili ili kujitangaza kimataifa zaidi.

“Tutumie lugha yetu ya kiswahili, mimi nina mjukuu wangu anajua lugha ya Kiingereza nikamuuliza unajua lugha wakati haujaenda hata shule, ila anatazama filamu za kizungu kujifunza, hivyo basi tuitumie lugha yetu kuwafundisha watoto walio Marekani ambao hawajui Kiswahili kupitia filamu zetu.”

Vile vile Professor Msando amewataka wasanii kusema ukweli kuhusu mali zao na pia kuhusu malipo wanayopata katika filamu hizo ili Waziri ajue.

“Wasanii semeni ukweli kuhusu mali zenu unakuta mtu anaigiza ana mali ila hana kitu mfukoni na analipwa kiasi kidogo sana anaogopa kusema kisa director atamnyima scene nyingine, pia wasanii acheni kuiga mambo ya ughaibuni utakuta stori mnarudia sana,” amesema Msando.

Hata hivyo Professor Msando ameiomba serikali kupitia Waziri Mwakyembe kujitahidi kuthamini lugha ya Kiswahili na kupitia filamu wanaweza kuwaalika wasanii kwenye ziara zao za nje kuweza kutambulisha kazi za hapa nchini kwani filamu inasaidia kuitambulisha nchi.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents