Burudani

Wasanii wa muziki nchini Uganda waungana kumtetea Bobi Wine, wamuomba Rais Museveni atumie busara za uongozi

Wasanii wa muziki nchini Uganda wameungana kwa pamoja mitandaoni kumshawishi Rais wa nchini hiyo Yoweri Museveni kumuachia huru mara moja msanii mwenzao wa muziki Bobi Wine ambaye pia ni Mbunge wa upinzani wa jimbo la Kyadondo.

Wasanii akiwemo Jose Chameleone, Eddy Kenzo, Vinka, Weasel, Juliana Kanyomozi, Irene Ntale na watu wengine maarufu nchini humo wametumia mitandao ya kijamii kumshawishi Rais Museveni kumuonea huruma Bobi Wine.

https://www.instagram.com/p/BmiuzlxBvDC/?taken-by=julianakanyomozi

https://www.instagram.com/p/BmiMk6CFtNF/?taken-by=jchameleon

https://www.instagram.com/p/BmiuzlxBvDC/?taken-by=julianakanyomozi

https://www.instagram.com/p/BmjbsUCARRr/?taken-by=irene_ntale

https://www.instagram.com/p/BmiKs1dnOzm/?taken-by=eddykenzo

Bobi Wine alikamatwa mjini Arua Uganda siku ya Jumatatu ya wiki hii na jeshi la polisi kwa kudaiwa kuwa alichochoa ghasia na kusababisha wananchi kuvamia msafara wa Rais Museveni aliyekuwa mjini humo kwa ajili ya kampeni za uchaguzi mdogo jimboni humo.
<blockquote><strong>SOMA ZAIDI -<a href=”http://bongo5.com/raia-wenye-hasira-waushambulia-kwa-mawe-msafara-wa-rais-museveni-mbunge-wa-upinzani-bobi-wine-akamatwa-kwa-uchochezi-08-2018/”> Raia wenye hasira waushambulia kwa mawe msafara wa Rais Museveni, Mbunge wa upinzani ‘Bobi Wine’ akamatwa kwa uchochezi</a></strong></blockquote>

Hata hivyo, ndugu wa rapa huyo mpaka sasa hawajui  yupo wapi ingawaje jeshi la polisi nchini humo linadai kuwa yupo hospitalini amelazwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents