Burudani

Wasanii wa Ukonga miyeyusho miyeyusha sana – Godzilla

Msanii wa muziki wa hip hop nchini, Godzilla amefunguka kwa kuwachana wasanii wenzake wanaoishi Ukonga Jijini Dar es Salaam kwa kuwaambia ni miyeyusho japokuwa ni ndugu zake wa kipindi kirefu na bado anawalea.

Zilla amesema hayo baada ya kuulizwa chanzo cha ugomvi wake na msanii Nikki Mbishi pamoja na Wakazi.

“Nikki ‘is my friend’ tumefanya kazi kwenye nyimbo yake, ‘I don’t know’ sijui kitu gani kimetokea lakini ‘we still friend. Mimi sina tatizo kwa sababu kama ingekuwa chochote kimetokea watu tusingefanya kazi pamoja, lakini imekuwa ‘too much’,” Zilla alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV.

“Unajua watoto wa Ukonga wengi wanakuwa miyeyusho miyeyusho lakini ni ndugu zangu wakina Wakazi, Nikki tunawalea tutafanyaje wanetu hao” aliongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents