Burudani ya Michezo Live

Wasanii wachanga wadai kulelewa na Sugar Mummy ni fursa kwenye muziki wao (Video)

Baadhi ya wasanii mkoani Tanga wameiambia Bongo5TV kwamba wapo baadhi ya wasanii wanalelewa na Wanamama wenye uwezo mkubwa wa kifedha maarufu kwa jina la MASHUGA MAMY katika Sanaa zao.

Mmoja ya wasanii chipukizi wa Bongo Fleva mwenye asili ya Mkoa huo wa Tanga, anaetamba na wimbo wake #KITU aliomshirikisha msanii, Belle9 anaefahamika kwa jina la @twiscoofficial amesema kuwa ni kweli wapo wasanii wanategemea nguvu kubwa kutoka kwa majimama wenye uwezo.

Muimbaji huyo ambaye anafanya kazi chini ya #KATEMI THE BOSS amesema kuwa ndoto yake kubwa ni kuwa mwakilishi mzuri wa Tanga kisanaa ya muziki.

Kwa upande wake Meneja wa msanii huyo aliefahamika kwa jina la @cieran7278 ameiambia @bongofive kuwa wanataka msanii wao apige hatua Zaid kisanaa ili mwisho wa siku aweze kujitegemea nje ya usimamizi wao.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW