Wasanii wajiunga kusaidia njaa..

Muungano wa wasanii kibao nyota wa miondoko mbalimbali ikiwemo Bongo Flava wako kwenye mazoezi makali kwa ajili ya kurecord albam ya pamoja ya kuchangia mfuko wa kupambana na tishio la njaa nchini.


Muungano wa wasanii kibao nyota wa miondoko mbalimbali ikiwemo Bongo Flava wako kwenye mazoezi makali kwa ajili ya kurecord albam ya pamoja ya kuchangia mfuko wa kupambana na tishio la njaa nchini.

Bushoke ni mmoja wa wasanii watakaokuwepo kwenye albam hiyo.

Akiongea hivi karibuni Mwenyekiti wa Mfuko wa Maafa,Imani Kajura…alisema kazi ya kurecord albam hiyo inafanywa ndani ya studio za Jag Records zilizoko Kinondoni na mpaka sasa wasanii kadhaa wameshaingia studio kwa ajili ya kazi hiyo.

Taarifa za karibu kutoka Jag Records zilisema kazi ya utengenezaji wa albam hiyo hata hivyo imekuwa ngumu kidogo kutokana na mgao wa umeme na hivyo kuwabidi wasanii wengi wafike kufanya kazi hiyo usiku.

Baadhi ya wasanii waliojitokeza kufanya albam hiyo ni pamoja na….. Ray C,
Bushoke, Juma Nature, Banana, Prof Jay, Lady Jay Dee, K-Bazil,
Bob Rudala na nyota wa taarab wa Zanzibar Stars Mzee Yusuph.

DHW inawapongeza wasanii wote waliojitokeza kufanya albam hii na hii inaonyesha ni jinsi gani wao kama wasanii wamekuwa mfano mzuri ambao utaweza kuwashawishi na wengine kujitolea chochote walichonacho kwa ajili ya kuchangia mfuko huu.

 

  • SOURCE: Darhotwire{mos_sb_discuss:10}

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW