Burudani

Wasanii wanapewa credit badala ya waandishi na waongozaji – Musa Banzi

Musa Banzi anaumizwa na kitendo cha wasanii kupewa credit badala ya credit hizo kupewa waandishi wa filamu na waongozaji.

musa banzi

Banzi amewahi kuandika filamu zilizowahi kufanya vizuri kama vile ‘Shumileta’, ‘Odama’ na nyingine nyingi.

Akizungumza kwenye kipindi cha E-News, kinachoruka kupitia EATV, Banzi alisema, ‘Siku hizi wasanii ndiyo wanaopewa credit kwenye movie badala ya madirector na waandishi. Watu wanatofautisha kati ya director, producer na msanii. Hata ukiangalia movie watu hawaangalii jina wala nani kaiandaa, watamsifia msanii aliyecheza utasikia Odama umefanya vizuri sana au Riyama umecheza vizuri sana,” aliongeza.

Kwa sasa mwandishi huyo anatarajia kufanya audition kwa ajili ya kuja na movie mpya ambayo itajulikana kama ‘Odama wa Dhahabu’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents