Burudani

Wasanii watano wa muziki wanaozidi kupanda chati kwa haraka kutoka pwani ya Kenya 2017

Hawa ni wasanii watano wa muziki wanaozidi kupanda chati kwa haraka kutoka pwani ya Kenya 2017.

1. SUDI BOY

Ni msanii ambaye amekuwa katika game ya muziki wa kizazi kipya kwa zaidi ya muongo mmoja kwa sasa. Mkali huyo wa muziki ambaye ana sauti inayoweza kumtoa nyoka pangoni, anatamba na kibao Iromo alichomshirikisha msanii kutoka Nairobi Timmy-tdat ambacho kinashikilia chati za vituo vya redio na television mbalimbali nchini Kenya.

Ana uwezo wa hali ya juu kenye muziki, na kila anapoachilia mzigo ni lazima mashabiki wake wafurahie. Katika kazi za awali alizowahi kutoa, zikiwemo Naona Bado aliomshirikisha msanii kidosho kwenye burudani ya mziki Amelina, Kule Kule, Kidonda, Mteja alichomshirikisha mtayarishaji wa muziki na muimbaji legendary Pilipili kutoka Nairobi, Barua kwa Rais aliomshirikisha gwiji wa muziki Afrika, Jaguar na vibao vingine vikali. Japo kwa hivi sasa Sudi amehamia jiji kuu la Kenya Nairobi, bado anawakilisha pwani ya Kenya vizuri kimuziki.

2. DOGO RICHIE

Haachi kuleta mjadala kwenye mitandao ya kijamii na vituo vya habari, kila wakati anapoachilia kazi zake. Hivyo wengi wamemfananisha na rapper mkali kutoka Bongo si mwingine bali Nay wa Mitego tofauti yao tu ni moja Nay anachana na kuimba mara nyingine lakini Richie yeye ni mwimbaji tu. Kwa sasa anatamba na kibao ”Mziki Majanga” ambacho kimekuwa gumzo nchini Kenya na kuvutia hisia mbalimbali huku wengine wakimkashifu na wengine kwa upande mwingine wakimsifu na kumtetea kuwa anafanya kadri ya uwezo wake kwenye sanaa ya mziki.

Vibao vyake alivyotangulia nikama vifatavyo; Ndani ya Moyo ft Sam wa Ukweli kutoka Tanzania, Sina raha, Naona Raha, Mziki ft Chikuzee, kibao hiki pia kilizua gumzo sana nchini Kenya, Yoyoba na vingine vingi.

https://www.youtube.com/watch?v=HFdd6zk_T4Y

3.OTILE BROWN

Staa wa muziki ambaye kulingana na twakimu za muziki nchini Kenya, inasemekana kwamba anapendwa sana na mashabiki wake haswa wakinadada. Na hii inatokana na kwamba nyingi ya nyimbo zake zina mahadhi ya kimahaba na jinsi anovyoitumia lugha ya Kiswahili kwa usanifu.

Mkali huyu ambaye kwa sasa anatamba na kibao Niseme Nawe alichomshirikisha Baraka Da Prince kutoka Bongo land, anazidi kutisha kimuziki kwani tokea angie kwenye hii game hajawahi kuwavunja moyo mashabiki wake. Vibao vyake vya awali nikama; Alivyonipenda alichomshirikisha rapper King Kaka kutoka Nairobi, Pakate, Dejavu alichomshirikisha rapper Kaligraph Jones kutoka Nairobi na vingine vingi. Otile brown anafananishwa na msanii wa merekani John Legend kwa mjibu wa gazeti maarufu la hapa nchini Kenya ”Daily Nation”.

https://www.youtube.com/watch?v=piC-Hipe5Ic

4. BROWN MAUZO

Mkali wa nyimbo Apotee ambayo pia mashabiki walimtuhumu kuWa alikua amemlenga ex-wake ambaye pia ni msanii maarufu Afrika mrembo Akothee. Akiongea na Mseto East Africa TV, Brown alikanusha tuhuma hizo na kusema nyimbo hiyo aliimuimbia mpenzi wake wa sasa na hakumanisha wala kufikiria kumlenga ex-wake.

Mwaka jana aliingia studio za Combination Sound pamoja na King wa Bongo flava mkali Alikiba na kuachilia ngoma kali kwa jina Nitulize. Ngoma nyingine alizowahi kuziachia awali ni pamoja na Natamani, Mapenzi maradhi aliyomshirikisha mkali wa Kokoro kutoka lebal yenye nguvu na ushawishi wahali ya juu barani Africa kwa sasa WCB, Rich Mavoko, Mke Mwema aliyomshirikisha mtayarishaji wa muziki na mwimbaji Bob Junior na nyingine nyingi.

https://www.youtube.com/watch?v=7S80VyrBIUc

5. SUSUMILA

Kwakweli hauwezi utaja muziki wa pwani ya Kenya bila kukosa kulipigia mstari jina la msanii legendary wa muziki wa kizazi kipya maarufu kaka Susumila. Amekuwepo kwenye game toka mwaka ya 1999 na hadi sasa bado yuko ngangari kama jinsi kibao chake cha awali alichomshirikisha mwanamuziki mwenza Escobar miaka mingi iliyopita. Susumila amekuwa kioo kwa waimbaji wengi kutoka eneo la pwani kwa jinsi alivyotikisa na anavyozidi kutisha kwenye hii game. Kwa sasa anatamba na kibao Ngoma Imezama ambacho kilitoka mwishoni mwa mwaka jana 2016.

Vibao vilivyomweka juu kwenye game hii ya muziki nikama vifuatavyo; Ngangari Kinoma, Hidaya, Ngoma itambe, Wewe alichomshirikisha Avril kutoka Nairobi, Mapepe alichomshirikisha rapper King Kaka kutoka Nairobi navingine vingine vingi.

Makala ya: Changez Ndzai (Kenya)
Facebook: Changez Ndzai
Instagram: changez_ndzai
Twitter : ChangezN

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents