Burudani

Wasanii wawili Mwana FA na Richie wateuliwa kuwa wajumbe wa bodi ya baraza la sanaa taifa (BASATA)

Wasanii wawili Mwana FA na Richie wateuliwa kuwa wajumbe wa bodi ya baraza la sanaa taifa (BASATA)

Wasanii wawili wa sanaa mmoja akiwa niĀ  mwanamuziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Hamisi M.Mwinjuma kwa jina maarufu la kazi Mwana FA pamoja na msanii wa Bongo Movie Single Mtambalike alimaarufu Richie wameweza kuwa miongoni mwa wajumbe watano walioteuliwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harison Mwakyembe.

Kufuatia uteuzi uliofanywa na rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli wa kumteua bwana Habbi Gunze kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) na leo Waziri mwenye dhamana ameweza kuteua wajumbe watano,miongoni mwa wajumbe hao wapo wasanii wawili ambao ni Mwana FA pamoja na Single Mtambulike – Richie.

Wengine walioteuliwa ni Mhadhiri wa Sheria Kitivo cha Sheria-UDSM, Dkt. Saudin J. Mwakaje, Mhadhiri Msaidizi Idara ya Sanaa-UDOM, Asha S. Mshana pamoja na Mhadhiri-UDOM, Dkt. Emmanuel M. Ishengoma, Uteuzi wa Wajumbe wote umeanza rasmi tangu Oktoba 05, 2018 na watatumikia Bodi kwa miaka mitatu.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents