Habari

Washikiliwa na polisi kwa kupatikana na samaki wachanga kilo 125

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu 18 kwa kupatikana na makosa mbalimbali ya kiuhalifu baada ya kufanyika kwa operesheni maalum wilayani Sengerema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Ahmed Msangi ameyasema hayo hii leo Agosti 4 mbele ya vyombo vya habari.

“Kwa siku mbili kuanzi tarehe 02.08.2018 hadi tarehe 03.08.2018 majira ya saa moja usiku kuanzia na kuendelea katika maeneo mbalimbali ya ndani ya ziwa Victoria na katika vijiji vilivyopo pembezoni mwa ziwa hilo wilaya ya Sengerema. Kulifanyika operesheni maalumu iliyoshirikisha kikosi maalumu cha askari polisi mkoa, polisi wanamaji (police marine) pamoja na askari polisi toka wilaya ya Sengerema,” amesema Kamanda Msangi.

Kamanda Msangi ameongeza “Kikosi hicho kilichoongozwa na Operesheni Afisa mkoa wa Mwanza, SSP Audax Majaliwa na Mkuu wa Polisi wilaya ya Sengerema, SSP Mairi Wassaga na kufanikiwa kukamata watuhumiwa 18 wa makosa mbalimbali ambayo ni kupatikana na samaki wachanga kilo 125, kupatikana na nyavu 50 za kuvulia samaki aina ya timba na kupatikana na bangi kilo 2.”

“Vilevile kupatikana na pombe ya moshi (gongo) lita 265, kupatikana na pikipiki moja izaniwayo kuwa ya wizi yenye namba mc 242 bdk na kupatikana na nyavu haramu 600 za kuvulia dagaa, vitendo ambavyo ni kosa la jinai.”

DCP Ahmed Msangi ameongeza kuwa  Polisi wapo katika upelelezi na mahojiano kwa watuhumiwa wote, ili kuweza kuwabaini wale wote wanaoishirikiana nao kwa namna moja au nyingine na uchunguzi ukikamilika watuhumiwa wote kumi na nane watafikishwa mahakamani.

Related Articles

3 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents