Promotion

Washindi wa Road To MAMAs wapatikana

 

Zaidi ya washindi watatu ambao ni kundi la pili walipatikana katika promosheni ya Road To Mama ambayo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika klabu ya usiku ya New Maisha Klabu.

{hwdvs-player}id=1233|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

Promosheni hiyo ambayo ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea kwenye tuzo zinazoandaliwa na kituo cha televisheni za burudani ya muziki Afrika MTV Base walipatikana baada ya kununua muda wa maongezi wa kuanzia shilingi elfu 5 na kusajiliwa kuingia katika bahati nasibu ya kupata washindi iliyofanyika katika klabu hiyo.

Washindi waliopatikana ni pamoja na mshindi wa kwenda kwenye party ya Road to MAMA DRC Congo, Mshindi wa Laptop aina ya Acer, Mshindi wa luninga aina ya Samsung na Mshindi pekee aliyejishindia tiketi ya kwenda kushuhudia fainali hizo za MAMA jijini Lagos nchini Nigeria ambaye atalipiwa kila kitu na Zain Tanzania.
Promosheni hiyo ilikuwa ni ya pili baada ya ile ya kwanza iliyofanyika katika ukumbi wa Thai Villageuliopo masaki  katika usiku wa B-Band iliyofanyika usiku wa tarehe 22 mwezi wa kumi.

Aidha kwa mujibu wa wandaaji promosheni zingine zinategemewa kufanyika na zawadi zaidi kutolewa ni pamoja na Via Via Club-Arusha, Villa Park-Mwanza, Club 84-Dodoma, 4Stars Club-Morogoro, na pati ya mwisho kubwa ya  Road to MAMA party ambayo itafanyika jijini Dar-Es-Salaam.

Ili kushiriki promosheni hiyo mteja wa zain atahitajika kununua vocha ya zain ambazo zitapatikana katika eneo la ukumbi na kupewa kuponi ambayo atakaa nayo hadi muda bahati nasibu ya kuchagua washindi itakapochezeshwa.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents