Picha

Washiriki Redd’s Miss Tanzania 2012 leo kuwania taji la Top Model jijini Arusha

Warembo 30 wanaowania taji la Redd’s Miss Tanzania 2012 leo oktoba 13, 2012 wanatarajia kupanda katika jukwaa la Naura Spring Hotel jijini Arusha kuwania taji la Top Model ambapo mshindi atapata tiketi ya kuingia nusu fainali ya Mashindano ya Miss Tanzania mwaka huu.

Shindano hilo lililopewa uzito kama fainali zenyewe linaandaliwa na Wandago Investment huku wabunifu mbalimbali wa mavazi wakionesha mavazi yao kupitia warembo wa Miss Tanzania.
Mkuu wa itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania, Albert Makoye amewataja wabunifu haokuwa ni Noel kutoka Dar es Salaam na Beate Allard na Marlies Gabriel kutoka Arusha.

Jumla ya warembo 30 wanaowania taji la Redd’s Miss Tanzania 2012, wapo katika ziara ya kutembelea vivutio vya utalii Kanda ya Kaskazini katika mikoa ya Arusha, Moshi na Manyara.

Mshindi wa shindano hilo la Top Model ataingia moja kwa moja katika hatua ya nusu fainali ya shindano hilo kubwa la urembo nchini Tanzania ambalo linadhaminiwa na Redd’s Premium Cold.

Mrembo huyo ataungana na Miss Photogenic 2012, Lucy Stephano na warembo wengine 15 watakao ingia hatua hiyo ya nusu fainali.

Msanii wa THT, Linah Sanga anatarajia kutumbuiza kwenye shindano hilo huku mchekeshaji wa kundi la Orijino Komede, Mpoki akiwa MC.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents