Michezo

Washiriki wa michuano ya French Open kuondoka na kitita kinono cha fedha

Mashindano makubwa ya mchezo wa tennis duniani maarufu kama French Open yametangazwa kuongezewa fedha kwa washindi watakao twaa tuzo katika kipindi cha majira ya Joto hadi kufikia pauni milioni 34.

Mchezaji tennis, Rafael Nadal 

Washindi wa pili wa tuzo hizo kubwa za grand slam ambazo zinatarajiwa kuanza Mei 27, kila mmoja atajiondokea na euro milioni 2.2 ambayo ni sawa na pauni milioni 1.9 kwa makadirio wakati kwa mwaka jana kilikuwa ni kiasi cha pauni 100,000 ambacho kimetolewa.

Kwenye ongezeko hilo kiasi kikubwa kimewekwa kwa wale wanaotoka mapema, waliyofanikiwa kufuzu hatua ya raundi ya tatu ambapo ni sawa na ongezeko la asilimia 20 wakati wale waliyofungwa raundi ya kwanza wakiondoka na euro 40,000  ambayo kwa makadirio ni sawa na pauni 35,000 ongezeko la karibu asilimia 15.

Mchezaji tennis, Latvia Jelena Ostapenko 

Kumekuwa na shinikizo kutoka kwa wachezaji wa mchezo wa tennis kuwa ni lazima tuzo hizo za  Grand Slams kuongeza thamani ya fedha ambnazo zilikuwa zikitoa hapo awali wakati rais wa wachezaji wa ATP, Novak Djokovic akiwa ameitisha mkutano wa siri na wachezaji kuzungumzia hilo huku, Roger Federer  akiamini kuwa wanastahili kupata kiasi kizuri cha fedha.

Mfuko wa tuzo za mchezo wa tennis katika michuano ya Australian Open kwa mwaka huu ni pauni milioni ni 30, wakati kwa mwaka jana mashindano ya Wimbledon walikuwa wakitoa pauni milioni 31.6 na US Open  ni pauni milioni 35.7.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents