Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Wasichana kufanya mapenzi kabla ya umri, Kwa muibua Waziri Ummy

Serikali kupitia Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewaomba Wabunge kuwasaidia kuhamasisha kuelimisha wasichana kujizuia kufanya mapenzi kabla ya utu uzima.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Wizara hiyo, Ummy Mwalimu leo Juni 13, 2018, Bungeni Jijini Dodoma ambapo amesema kuwa asilimia 27 ya watoto wa kike wamepata ujauzito kabla ya umri wa miaka 18.

“Suala la mimba za utotoni nakubaliana kwamba ni changamoto, asilimia 27 ya watoto wa kike wamepata ujauzito kabla ya umri wa miaka 18 kwahiyo katika mpango wetu wa kuhimiza kwahiyo katika mpango wetu wa kuhimiza kuzuia mimba za utotoni especially katika Mikoa ya Katavi tumeamua kutumia njia ya kuwaelemisha wasichana wajizuie kuingia katika vitendo vya ngono mpaka pale watakapo fikisha umri wa miaka 18,” amesema Ummy.

“Kwa kweli hali sio nzuri watoto wetu wa kike wanaanza ngono asilimia 14 ya watoto wa kike wanaanza ngono kabla hawajafikisha umri wa miaka 15 na watoto wa kiume ni asilimia tisa kwahiyo niwaombe wabunge mtusaidie katika kuhamasisha na kuelimisha wasichana kujizuia kufanya mapenzi kabla ya utu uzima,” amesititiza.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW