Habari

Wasichana msikubali kuolewa na wanaume wenye viwanja mabondeni – RC Makonda (Video)

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewataka wanawake wa mkoani humo kutokubali kuolewa na wanaume ambao wanaviwanja mabondeni.

RC Makonda ametoa kauli hiyo leo wakati alipofanya ziara ya kukagua uharibifu wa nyumba zilizovunjika eneo la Kingugi kwa Mnyani Kata ya Kilungule baada ya wakazi kujenga kwenye maeneo yasiyoruhusiwa.

Aidha RC Makonda amewaagiza Wenyeviti wote wa mitaa kuainisha nyumba zilizojengwa kwenye maeneo hatarishi ambapo amewataka kutoruhisu watu kujenga maeneo ya mabondeni.

Katika kutafuta mwarobaini wa tatizo la wananchi waishio mabondeni RC Makonda ameandaa mkutano wa wananchi wote waishio maeneo ya mabondeni kwaajili suluhisho la kudumu.

Katika ziara alizofanya RC Makonda amejionea nyumba nyingi zikiwa zimejengwa kwenye maeneo yasiyo rasmi kiasi kwamba hata ikitokea janga la moto inakuwa vigumu Jeshi la zimamoto na uokoaji kufika na hata mgonjwa akizidiwa gafla ni vigumu kuwahishwa hospital jambo ambalo ni hatari kwa usalama.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents