Bongo5 Exclusives

Wasichana 8 wapya watakaoupeleka muziki wa Tanzania kimataifa

Tukiwa tupo mwezi wa tatu tu tangu mwaka 2013 uanze, tayari dalili zinaonesha kuwa huu ni mwaka wenye ushindani mkubwa zaidi kimuziki kuliko miaka yote. Ni mwaka ambao wasanii wana take risk zaidi kwa kuwekeza zaidi kwenye muziki wao ikiwa ni pamoja na kufanya video kwa gharama yoyote inayowezekana. Ushindani ni mkubwa kiasi ambacho kwa sasa kinachofanya ngoma ifanye vizuri si jina la msanii bali ni utamu, uzuri na ubora wa kazi yenyewe hata kama ni msanii mpya kabisa.

Mwishoni mwa mwaka 2012 na mwanzoni mwa 2013, kumetokea mwamko wa aina yake wa wasanii wa kike wanaofanya muziki uoonesha matumaini ya kuipelekea Tanzania next level. Mwamko huo umeuchangamsha zaidi muziki wa Tanzania hasa kwakuwa wasanii wa kike ni wachache. Pamoja na kuwepo wasichana kadhaa wapya wanaojaribu kutoka, hawa wafuatao tunaamini wana quality zaidi za kimataifa kutokana na muziki wanaoufanya na jinsi walivyokuwa exposed.

Vanessa Mdee

Vanessa-Mdee

Vanessa Mdee alimake headline sana aliposhirikishwa na Ommy Dimpoz kwenye Me and You iliyotoka mwishoni mwa mwaka jana. Sauti tamu kwenye chorus hiyo iliwashtua wengi kwakuwa alikuwa akijulikana kama mtangazaji tu. January mwaka huu aliachia single yake ya kwanza Closer. Ngoma hiyo ilipokelewa positively na miongoni mwa nyimbo zilizopata downloads nyingi zaidi mtandaoni. Kwenye uzinduzi wa wimbo huo, Vanessa alisema, “ It’s nice kuna watu positive watu wanaosupport movement so am really excited they are here, bado tuko mwanzo, it’s very interactive, najua ni kitu ambacho hakijafanyika Tanzania before so napenda kuwa intimate na fans wangu, those people who are listening to the music, wana support, wanadownload , kujua maoni yao juu ya nyimbo so that why nimefanya hiki kitu.”

Vanessa aIisema sababu ya kuachia wimbo wake mwenyewe kipindi hicho hakikutokana na jinsi watu walivyomkubali kwenye collabo alizofanya bali huo ni mpango uliokuwepo kwa muda mrefu.

http://www.youtube.com/watch?v=FkNzhUJwUvc

“Market ya Tanzania ni kama haitabiriki, so I was a bit sceptical but namshukuru Ommy Dimpoz kwa kunishirikisha kwenye nyimbo yake pamoja na AY. Wao wanasimama peke yao lakini ni kama favour wamenipa kamba nicollaborate nao and I am grateful for that forever kwasababu wameniintroduce kwa audience yao.”

Hivi karibuni aliachia remix ya Closer aliyowashirikisha Gosby na Ommy Dimpoz. Video yake huenda ikaanza kutayarishwa hivi karibuni. Jumatatu hii ametweet, “Looking for females in Tanzania 18+ who look hella hella on camera and can dance, are you that somebody – hit up my lady @MzzAbby.”

Maua Sama

Maua Sama ni msanii chipukizi kutoka Moshi. Ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Cha Ushirika na Biashara Moshi.

Maua ni almasi mchangani ambayo imegunduliwa na MwanaFA baada ya kupata ‘demo’ yake aliyofanyia studio za Moshi na kuipeleka mbele ya “Management Team” yake Lifeline/T.I.A ambao moja kwa moja wakamchukua. Maua anafanya kazi chini ya uangalizi wa Lifeline/T.I.A Inc; Label ya muziki ambayo inasimamia kazi za muziki za MwanaFA. So Crazy ambao ni wimbo wake wa kwanza umetayarishwa na producer Marco Chali wa MJ Records na amemshirikisha MwanaFA. Mipango iliyopo ni kumfanya Maua Sama kuwa mwimbaji bora wa muziki Tanzania.

[soundcloud url=”http://api.soundcloud.com/tracks/79048750″ params=”” width=” 100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Feza Kessy

62463_10152632992750473_172344653_n

Feza Kessy aliwahi kuwa Miss Dar City Centre. Baada ya kushiriki Miss Tanzania alienda masomoni nchini Uingereza ambako alifanikiwa pia kupata mtoto wa kiume. Baada ya kurudi Tanzania aliamua kuifufua ndoto yake ya kufanya muziki kwakuwa alikuwa nayo hata kabla ya kushiriki Miss Tanzania.

“Kwanza mimi napenda kusema nilienda Miss Tanzania my passion was singing,” alilimbia jarida la Mzuka mwaka jana. “Nilienda pale kuonesha talent yangu ya kuimba ili nionekane. So that was my aim kwasababu nilijaribu kwenda kwa different producers na nini, na kama unavyojua the game ni ngumu, it’s very hard, ikawa ngumu kwa mimi kubreakthrough to even get a producer who would work with me. Lakini wale watu wa miss walivyoniapproach mimi, to me was like I am beautiful let me use this opportunity to get what I want.”

[soundcloud url=”http://api.soundcloud.com/tracks/78748109″ params=”” width=” 100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Na sasa akiwa na single kali hewani, Amani ya Moyo, Feza ana kila dalili za kufanya vizuri kimataifa kwakuwa yupo chini ya kampuni ya AY, Unity Entertainment ambayo inahusika na kusimamia kazi zake.


Shosteez (Menynah, Salma na Nuru)

http://www.youtube.com/watch?v=EdvDvo99etE

Baada ya kuona uwezo wa Menynah Atick na Salma Mahin kwenye Bongo Star Search mwaka jana, producer Lamar wa Fish Crub aliona anaweza kufanya kitu na wasichana hao warembo. Aliamua kuunda kundi la wasichana watatu alilolipa jina Shosteez na kumuongeza Nuru.

Wakiwa na muda mfupi tu tangu wawe pamoja, kwa sasa Shosteez wameshaanza kumake headline na video yao kali ya On the Floor. Kuna taarifa pia kuwa hivi karibuni wataonekana kwenye tangazo la kinywaji kikubwa duniani. Muonekano wao wa kimataifa unawapa uhakika wa kuwa na mustakabali mzuri katika muziki na ni wazi kwa muziki wao, Shosteez ni Unique Sisters wapya.

Eslyne Eberts

Eslyne_700_2

Eslyne Erastus Eberts, alizaliwa December 18, 1991 jijini Arusha Tanzania. Alihamia Birmingham Alabama mwaka 1994 na wazazi wake pamoja na dada zake wawili na kurudi Arusha mwaka 1999 na mpaka sasa anaishi Sakina, Arusha. Ni mtoto wa mwisho katika watoto sita akiwa na dada watatu na kaka wawili.

Eslyne alianza kuvutiwa na muziki akiwa na umri wa miaka mitano aliposikia wimbo “Forever,” na “If you ever need a friend” za Mariah Carey.

Tangia hapo alianza kuimba akiwa na umri mdogo kwenye matamasha ya shule na kwaya ya kanisa. Ni muimbaji na mtunzi wa rnb, Afro-pop, techno, sweet reggae, na rap. Akiwa na miaka kumi na, ameshawahi kutunga nyimbo za kanisa analosali la Heritage of faith Christian centre- Arusha linaloongozwa na baba yake wa kumuasili (adoptive father) Pastor Gary. J. Eberts. Msichana huyu mrembo ni shabiki mkubwa wa Stevie Nicks, Maria Carey, and Keri Hilson.Pia kwa Tanzania anampenda zaidi Lady Jaydee.

Kwa Profession , Eslyne amesomea na ana uzoefu wa masuala ya media. Anasimamiwa na Borry Mbaraka, Manager wa Tripple A FM waliokutana miaka kadhaa iliyopita na kufanya naye vipindi mwaka 2011.

Kwa sasa anafanya kazi za muziki kadhaa na studio ya Noizmekah records ya Arusha Tanzania, na tayari ameshatoa wimbo uitwao “Pride down”, uliotayarishwa na Def-xtro, producer maarufu nchini ambaye Eslyne anamzungumzia kama si producer tu mzuri bali rafiki ambaye amempa moyo na kumsupport kukuza kipaji chake kimuziki.

Tanah

tana

Jina alilopewa na wazazi wake ni Happy Jaffari Kalinga. Ana pacha wake wa kiume aitwaye Alex Jaffari Kalinga. Anaunda kundi liitwalo Tanchy akiwa na Chibwa ambaye pia ni mpenzi wake. Kabila lake ni mhehe na alizaliwa mwaka 1990 katika hospitali ya Aga khan jijini Dar es Salaam. Shule ya msingi amesoma St Mary’s mpaka sekondari na kumalizia Happy Skillful Secondary mwaka 2008. Chuo amesema DJS mpaka level ya Diploma. Alianza muziki mwaka 2007 akiwa kidato cha nne.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents