Habari

Wasioamini uwepo wa Mungu Kenya wataka kuondolewa neno ‘God’ kwenye wimbo wa taifa

Chama cha watu wasioamini uwepo wa Mungu (Atheists) nchini Kenya kimetaka kuondolewa kwa neno ‘God’ kwenye wimbo wa taifa.

maxresdefault

Wanadai kuwa neno ‘God” kwenye mstari wa kwanza wa wimbo huo halihimizi moyo wa umoja kwakuwa si Wakenya wote wanaomuamini Mungu.

Wamedai kuwa Kenya ni nchi isiyo na dini na hivyo kuimba wimbo wa taifa wenye neno ‘God’ inakinzana na katiba ya nchi hiyo. Wimbo wa taifa wa Kenya huanza na kwa kusema “Oh, God of all creation.”

Watu hao wamesema kuwa huhisi kutengwa kila wimbo huo unapoimbwa. Wamesema watapeleka malalamiko yao bungeni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents