Habari

Wasiwasi watanda kati ya Marekani na Iran Donald Trump asema ” Tukipigana na Iran itakuwa mwisho wa taifa hilo”

Rais wa Marekani Donald Trump ameionya Iran kwamba itaharibiwa iwapo vita vitazuka katika ya mataifa hayo mawili. ”Iwapo Iran inataka kupigana , huo nduo utakuwa mwisho rasmi wa taifa hilo” , alisema katika jumbe wa Twitter siku ya Jumapili. ”Musijaribu kuitisha Marekani tena”. Ujumbe huo wa Twitter wa bwana Trump unaadhimisha kubadilika kwa msimamo baada ya jaribio la hivi karibuni la la kuficha uwezekano wa vita kati ya mataifa hayo mawili.

Kwa mujibu wa BBC. Siku chache zilizopita , rais huyo aliwaambia washauri wake kwamba hapendelei shinikizo ya Marekani dhidi ya Iran kubadilika na kuwa vita.

Na alipoulizwa na waandishi wa habari siku ya Alhamisi iliopita iwapo Marekani ilikuwa ikijiandaa kivita , bwana Trump alijibu: Sidhani.

Iran pia imepinga madai ya kuwepo kwa hali ya wasiwasi. Siku ya Jumamosi waziri wa maswala ya kigeni wa taifa hilo Javad Zarif alisema kuwa hakuna hamu ya Vita.

”Hakutakuwa na vita kwa kuwa hatutaki vita na hakuna mtu ambaye anafikiria kuivamia Iran katika eneo hili”, Mohammed Javad Zarrif aliambia chombo cha habari cha Irna.

Meli ya Kivita ya Marekani ikielekea katika eneo la Ghuba

Kwa nini kuna wasiwasi?

Msuguano huo wa hivi karibuni unajiri baada ya Iran kusitisha kwa muda majukumu yake iliofaa kuyafuata chini ya mpango wa kinyuklia wa 2015, na kuonya kuendelea kuzalisha madini ya Uranium ambayo hutumika kutengeza mafuta na silaha za kinyuklia.

Mpango huo ulilenga kusitisha vikwazo dhidi ya Iran na badala yake Iran isitishe mpango wake wa Kinyuklia, lakini Marekani illijiondoa katika makubaliano hayo mwaka uliopita.

Akiyataja makubaliano hayo kuwa mabaya, bwana Trump baadaye aliiwekea vikwazo Iran.

Tehran imedaiwa kubeba silaha katika maboti katika eneo hilo la mashariki ya kati, na wachunguzi wa Marekani wanaamini kwamba taifa hilo lilishambulia meli nne za mafuta katika pwani ya UAE madai ambayo Iran imekana.

Kiongozi wa kidini nchini Iran Ayatollah Ali Khamenei (kushoto) na mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin SalmanHaki miliki ya pichaREUTERS

Ni kipi kipya katika eneo la mashariki ya kati?

Katika siku za hivi karibuni Marekani imepeleka meli ya kivita inayobeba ndege kwa jina USS Abraham Lincoln katika eneo hilo na imedaiwa kuwa kuna mpango wa kuwatuma wanajeshi 120,000 katika eneo hilo.

Wafanyikazi wa Kidiplomasia wametakiwa kuondoka nchini Iraq, na jeshi la Marekani limepandisha viwango vya hali ya tahadhari katika eneo hilo kutokana na ujasusi kuhusu vikosi vinvayoungwa mkono na Iran- hali inayokiuka madai ya jenerali mmoja wa Uingereza anayesema kuwa hakuna hali yoyote ya vitisho ilioongezeka.

Wanajeshi wa Uholanzi na wale wa Ujerumani wanasema kuwa wamesitisha mazoezi yao ya kijeshi katika taifa hilo.

Siku ya Jumapili , jeshi la Iraq lilisema kuwa roketi ilirushwa katika eneo salama linalolindwa sana katika mji wa Baghdad ambalo linamiliki majumba ya serikali na balozi za kigeni.

Inadaiwa kuwa roketi hiyo ilipiga jumba moja lililowachwa karibu na ubalozi wa Marekani.

Hakuna majeraha yoyote yalioripotiwa na haijulikani ni nani aliyehusika na shambulio hilo.

Kwengineko, Saudia imeishutumu Tehran kwa kutekeleza shambulio la ndege isiokuwa na rubani katika bomba moja la mafuta siku ya Ijumaa. Inadaiwa kuwa waasi wa Houthi walitekeleza shambulio hilo kupitia maagizo ya Iran. Gazeti moja la Saudia linalounga mkono serikali ya taifa hilo lilitoa wito kwa Marekani kulishambulia taifa hilo. Iran denies the allegations. Marekani imepeleka meli zaidi za kivita na ndege katika eneo la mashariki ya kati katika siku za hivi karibuni.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents