Bongo Movie

Wastara: Sajuki aliondoka na nusu ya akili yangu

Muigizaji wa filamu, Wastara Juma Sajuki amesema pengo la mume wake Sajuki halijazibika.

Sajuki Na Wastara
Sajuki Na Wastara

Sajuki alifariki January 2, 2013.

“02.01.2015 Marehemu mume wangu kipenzi Juma Kilowoko (sajuki)anatimiza miaka 2 tangu atuache tukiwa na majozi tele moyoni mwetu,” ameandika Wastara kwenye Facebook.

“Ni ukweli usipoingika ameondoka na nusu ya akili yangu maana sifanyi chochote bila kumfikilia yeye kwa jinsi alivyokua na mawazo mazuri ya kujenga namkumbuka na nitamkumbuka siku zote za maisha yangu,nampenda na nitampenda siku zote.

Hivyo 02.01.2015 kutakuwa na dua itakayosomwa kwenye kaburi lake kisutu Dar es salaam kuanzia saa nne asubuhi,na badae kutakuwa na dua nyumbani tabata pamoja na chakula cha mchana kwa watakaojaliwa naomba tuungane pamoja kwenye dua hii,asanteni nawapenda wote.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents