Habari

Wataalamu wa anga wagundua maji sayari ya mbali, muongozaji wa utafiti huo adai hata hewa yake ni rafiki kwa viumbe hai

Kwa mara ya kwanza wataalamu wa anga wamegundua maji katika sayari inayozunguka katika nyota iliyoko orbiti yenye mazingira sawa na yaliyo duniani.

K2-18b

Utambuzi huo unaifanya sayari inayotambulika kwa lugha za kisayansi K2-18b kua ni moja ya sehemu zitakazofanyiwa utafiti juu ya viumbe wanaoaminika kuwepo duniani ‘aliens’.

Ndani ya miaka kumi kuanzia sasa, darubini mpya ina uwezo wa kutambua kama anga za sayari K2-18b ina gesi ambazo zina uwezekano kua zilitokana na viumbe hai.

Taarifa hizo zimeandikwa na jarida la kisayansi la ‘Nature Astronomy‘.

Prof. Giovanna Tinnetti, mwanasayansi aliyeongoza watafiti kutokea chuo cha London (UCL), ameeleza kuwa ugunduzi huo ni mkubwa.

“Hii ni mara ya kwanza kwa maji kugunduliwa kwenye sayari yenye hali sawa na dunia, katika nyota hii ambayo hali ya hewa yake ni rafiki kwa maisha ya viumbe hai”Profesa alifafanua.

Sayari hii mpya ina ukubwa mara mbili ya dunia na katika kundi lake inajulikana kama “Super Earth” na ina hali ya hewa inayoweza kuruhusu maji au kimiminika kuanzia nyuzi joto sifuri mpaka.

Sayari ya K2-18b yenye umbali wa maili millioni 650 kutoka duniani ni miaka 111 kwa spidi ya mwanga, hivyo ni ngumu kutuma kifaa huko

Hivyo nafasi pekee ya kuitambua zaidi ni kusubiri kwa kizazi kijacho cha wana anga kuitambua zaidi sayari hiyo hasa kwa darubini mpya itakayozinduliwa kuanzia miaka ya 2020.

Timu ya wanasayansi iliyogundua ilipitia sayari zilizogunduliwa na Hubble Space Telescope kati ya mwaka 2016 na 2017 na ndipo walipoigundua K2-18b kuwa ina uwezo wa kuwa na maji.

Wana-anga wengine wanapingana na taarifa hiyo juu ya uwezekano wa viumbe wengine kuishi.

Utafiti mmoja ulionesha kua sayari ambazo zina uzito mara moja na nusu zaidi ya ule wa dunia zina uwezekano mdogo wa kua na sura yenye miamba.

Hivyo kuna wasiwasi kama nguvu ya mvutano ya sayari K2-18b’s itaweza kuwa rafiki kwa viumbe hai

K2-18b haiwezi kuchukuliwa kama sayari iliyodumaa, ina sifa zaidi za kuifanya kua sayari kutokana na kua na miamba ya ndani na theluji.

Aina hii ya sayari hutambulika kama sayari bahari, mtafiti huyo aliiambia BBC

“Kwa sasa hatuwezi kusema kama sayari hii ina bahari katika miamba yake kutokana na utafiti uliofanywa sasa ila kutambua kama kuna maji katika eneo lake ni mwanzo mzuri” mtafiti Dkt Angelos alisema.

Huku hili likiwa wazo ambalo Dkt. Laura kreinberg kutoka kituo cha wanaanga katika chuo cha Havard hakubaliani nalo.

Artwork of Ariel

“Sayari hii ina sifa nyingi zaidi za sayari ya Neptune.

Mkandamizo na hali ya hewa inaongezeka kutokana na kina, hivyo kuna ugumu kwa vitu vya dunia vinavyowezekana duniani kufanyika kutokana na joto kali na mgandamizo mkubwa wa hewa ulioko kwenye sayari hiyo” aliiambia BBC Dr. Laura kreinberg .

Prof. David Charbournneau pia kutokea chuo cha Havard aliongeza kua ugunduzi wa anga la sayari K2-18b’s hi kiashiria tosha kua haiwezi kuwa na uwezo wa viumbe hai kuishi.

Aliongeza kua kama sayari ingekua na anga nene inayofanana na la dunia basi ‘telescope ya hubble’ isingeweza kuigundua hivyo jambo hilo linaongeza mashaka kwake kama viumbe wanaweza kuishi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents