Habari

Watafiti wa ugonjwa wa Zika wakiri kuwa virusi hivyo ni hatari zaidi

Wanasayansi kutoka nchini Brazil wanaoendelea kuchunguza ugonjwa wa Zika unaonekana kuwa ni hatari zaidi tofauti na mwanzo walivyofikiria.

160305041013_brazil_microcephaly_baby_512x288_ap_nocredit

Ugonjwa huo unasababishwa na virusi vya Zika ambavyo vinasababisha kuzaliwa kwa watoto wakiwa na vichwa vidogo.

Wakiongea na BBC, madaktari hao bingwa wamesema kuwa virusi vya Zika vinaweza kuwa sababu ya kutokea kwa matatizo ya neva za fahamu kwa mwanamke mmoja mjamzito kati ya watano wanaoathiriwa na Virusi hivyo.

Mwanzoni maafisa kutoka CDC waliripoti kuwa virusi vya Zika huenezwa na mbu lakini njia nyingine ambayo unaweza kuambukizwa ni kufanya mapenzi. Watafiti wa ugonjwa huo sasa wameanza kukukubali kuwa kuna uhusiano kati ya mbu anayeeneza virusi na tatizo la watoto kuzaliwa na dosari kwenye ubongo.

Madaktari nchini Brazil wameiambia BBC kuwa asilimia ishirini ya mimba zilizoathiriwa na ZIKA zitasababisha aina nyingine ya kuharibiwa kwa ubongo wa mtoto akiwa tumboni.

Watafiti hao wamesema kuwa asilimia moja ya wanawake walioathiriwa na virusi vya Zika wakati wa ujauzito kuelezwa kuwa watapata watoto wenye vichwa vidogo.

Bado watafiti wanaendelea kutafuta chanjo ambayo itasaidia kupunguza kasi ya ugonjwa huo ambao umeenea zaidi bara la Amerika Kusini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents