Tupo Nawe

Watafiti wamebaini kuwa aina ya binadamu wa kwanza anayefanana na binadamu wa sasa alitoka nje ya Afrika, waitaja sehemu hii

Watafiti wamebaini kuwa aina ya binadamu wa kwanza anayefanana na binadamu wa sasa alitoka nje ya Afrika

Watafiti wamebaini kuwa aina ya binadamu wa kwanza anayefanana na binadamu aliyepo wakati huu alitoka nje ya Afrika. Fuvu lillilofufuliwa nchini Ugiriki limegunduliwa kuwa ni la binadamu aliyeishi miaka 210,000 iliyopita, wakati ambapo Ulaya ilichukua aina ya kizazi cha binadamu kilichojulikana Neanderthali

Kwa mujibu wa BBC. Uvumbuzi huu wa kusisimua unaongeza ushahidi wa awali wa uhamiaji wa watu kutoka bara la Afrika ambao ulisababisha kutopatikana kwa vinasaba ama DNA za watu wanaoishi sasa

Matokeo ya uvumbuzi huu yamechapishwa katika jarida la masuala asili.

Watafiti wamefichua mafuvu ya binadamu hao kwenye pango la Apidima nchini Ugiriki katika miaka ya 1970.

Moja ya mafuvu hayo lilikuwa limeharibika lakini jingine lilikuwa kamili, na ilibidi utumiwe mtambo wa kompyuta kuchunguza na vipimo kadhaa vya uranium vinavyobashiri tarehe kufichua taarifa kuhusu mafuvu hayo.

Fuvu lililokuwa kamili lilionekana kuwa ni la aina ya binadamu wa Neanderthali. Lakini jingine lilionyesha tabia wazi, kama vile muundo wa duara kwenye sehemu ya nyuma ya fuvu, ambalo ni sawa na lile tulilonalo binadamu wa sasa.

Masalia ya binadamu wa kale wa Afrika

Zaidi ya hayo, fuvu la Neanderthali lilikuwa ni la mtu aliyekuwa na umri mdogo.

Kile tulichokishuhudia ni kwamba nchini Ugiriki walikuwepo na kikundi cha watu wa kizazi cha binadamu kinachofanana na cha sasa mapema zaidi nchini Ugiriki miaka 210,000 yiliyopita, chenye idadi ambayo labda inaweza kulinganishwa na watu wa Levant, lakini nafasi yao ikachukuliwa na binadamu wa aina ya Neanderthali yapata miaka 170,000 iliyopita,” amesema mtafiti mwenza Profesa Chris Stringer, kutoka katika kituo cha Makumbusho ya Historia ya masuala ya asili mjini London.

Watu wanaoishi nje ya Afrika leo wanawapata mababu zao wa kale katika vizazi vilivyoondoka katika bara hilo miaka 60,000.

Watu wanaoishi nje ya Afrika leo wanawapata mababu zao wa kale katika vizazi jvilivyoondoka katika bara hilo miaka 60,000.
Image captionWatu wanaoishi nje ya Afrika leo wanawapata mababu zao wa kale katika vizazi jvilivyoondoka katika bara hilo miaka 60,000.

Huku binadamu wa sasa wakiishi katika maeneo ya Ulaya na Asia, wamechukua kwa kiasi kikubwa nafasi ya jamii za binadamu wengine kama vile Neanderthali na Denisovani.

Lakini huu haukuwa uhamiaji wa kwanza wa binadamu wa kisasa (au Homo sapien) kutoka Afrika.

Mafuvu ya Homo sapieni kutoka maeneo ya Skhul na Qafzeh nchini Israel yaliyobainika miaka ya 1990 yaliiishi kati ya miaka 90,000 na 125,000 iliyopita.

Hata hivyo, katika miaka ya hivi karibuni, imekuja kutambuliwa kuwa vizazi vya binadamu wa kale viko nje ya Afrika mapema hata zaidi na zaidi ya ilivyoaminiwa awali.

Katika miaka michache iliyopita, wataalam wa uvumbuzi wa muundo na mabadiliko ya mafuvu ya binadamu kutoka Daoxian na Zhirendong nchini Uchina walisema mafuvu hayo ni ya binadamu walioishi kati ya 80,000 na 120,000 iliyopita.

Uchunguzi wa DNA ulibaini ishara za mchanganyiko wa vizazi vya binadamu wa Afrika na Neanderthali. Ushahidi kutoka wa binadamu wa kizazi cha Ujerumani cha Neanderthali unaonyesha kuwa mchanganyiko huo ulitokea baina ya miaka 219,000 na 460,000 , ingawa haijabainika wazi ikiwa kizazi cha binadamu wa kale cha Homo sapieni kilihusika, au kikundi kingine cha Waafrika wa kale.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW