Habari

Watakaobainika kuwapa ujauzito wanafunzi kukiona chamoto

Watakaobainika kuwapa ujauzito wanafunzi kukiona chamoto

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imeweka sheria kali zinazowalinda watoto wa kike na watakaobainika kuwapa ujauzito na kukatisha masomo yao adhabu watakayoipata hawatoisahau maisha.

Majaliwa ameyasema hayo hapo jana siku ya Jumapili ya Julai 29, 2018 wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Mwakizega wilaya ya Uvinza akiwa katika  ziara yake ya kikazi mkoani Kigoma.

Alisema Serikali itatoa adhabu kali kwa mtu atakayebainika kukatisha elimu ya mtoto wa kike iwe kwa kumuoa au kumpa ujauzo huku akiongeza kuwa watoto wa kike wanatakiwa kuheshimiwa katika jamii na waachwe waendelee na masomo yao kwani elimu ni haki yao ya msingi.

“Tukikukuta na mwanafunzi wa kike kwenye kona zisizoeleweka adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka 30 gerezani, hivyo vijana kuweni makini,” alisisitiza.

Pia Waziri Mkuu aliwataka wazazi na walezi kushirikiana na Serikali kuhakikisha watoto wa kike wanapelekwa shule na wanamaliza masomo yao.

Waziri Mkuu aliwaasa wanafunzi wote kusoma kwa bidii ili watimize ndoto zao na wasikubali kushawishika kwa kuwa watashindwa kufikia masomo yao.

Related Articles

9 Comments

  1. Nitaozea jela mm jaman atangeludixhwa nilipotoka nikazaliwa upya nafikixha mwaka nipojela hata hivyo ncngetoboa jaman nitafutien mganga au kama kunamtu babuyake mganga ama ndugu yake anixaidie ncendejela mm

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents