Habari

Watano wapoteza maisha Kenya kwenye mapokezi ya Raila Odinga

Imeripotiwa kuwa takriban watu watano wamepoteza maisha jijini Nairobi nchini Kenya na wengine kujeruhiwa wakati polisi nchini humo ikikabiliana na wafuasi wa kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

Maelfu ya wafuasi wa upinzani leo walikusanyika katika uwanja wa ndege kumpokea Raila Odinga ambaye alikuwa anarejea kutoka nchini Marekani.

Msemaji wa jeshi la polisi nchini humo, George Kinoti amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kusema kuwa vimetokana na mkanyagano wa Wafuasi hao na sio nguvu ya polisi kama inavyoelezwa.

Taarifa kutoka Shirika la Utangazaji la Reuters zimeeleza kuwa Polisi walirusha mabomu ya machozi na vilipuzi kuwatawanya wafuasi hao huku gari moja la polisi likichomwa moto.

Raila Odinga alisusia kushiriki marudio ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 26 huku akitaka uchaguzi huo kuahirishwa kwa mara ya tatu lakini Tume ya Uchaguzi nchini humo ilikataa kufanya hivyo.

Jumatatau ijayo Mahakama ya juu nchini Kenya inatarajiwa kutoa uamuzi wake kuhusu uhalali wa uchaguzi wa tarehe 26 Oktoba ambao rais Uhuru Kenyatta alibuka mshindi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents